Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan
anatarajiwa kuongoza Kampeni ya kunusuru Bonde la Mto Ruaha Mkuu
lililopo Iringa kutokana uharibifu mkubwa unaendelea, huku akiambatana
na Mawaziri watano ambao watasaidia kuokoa uharibifu wa Mazingira.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na
Mazingira, Januari Makamba alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari
jana Jijini Dar es salaam.
Alisema
kuwa Ofisi hiyo imeanzisha Kampeni hiyo kwa sababu Hifadhi ya Bonde la
Mto Ruaha Mkuu ni kubwa kuliko yote hapa Afrika Mashariki.
Alisema
kuwa uharibifu unafanywa kutokana na shughuli mbalimbali za kibinadamu
katika Bonde hilo unasababisha kukauka kwa Mto Ruaha ambao ni tegemezi
katika nyanja za kiuchumi.
Aidha,
Makamba aliwataja Mawaziri watakaoongozana na Makamu wa Rais kuwa ni
pamoja na Waziri wa Maji, Gerson Lwenge, Waziri wa Ardhi, William
Lukuvi, Waziri wa Maliasili na Utalii, Jumanne Maghembe, Waziri wa
Kilimo, Charles Tizeba.
Vile
vile, aliongeza kuwa hali ya mazingira kwa sasa ni mbaya sana kwenye
bonde hilo kwani ukifika wakati wa kiangazi mto huo wa Ruaha Mkuu
hautirirshi tena maji kama ilivyokuwa zamani.
“Hali
hii inasababisha kupungua kwa watalii, shughuli za kiuchumi na
uzalishaji wa umeme ambao unamrahishia mwananchi wa kawaida kupata umema
nafuu, pia uhalibifu huu wa Mazingira unahatarisha maisha ya wanyama,”alisema Makamba.
Hata
hivyo alitoa wito kwa wananchi wote kutunza vyanzo vya maji, Mazingira
ili viweze kuwaletea manufaa kwa sasa na vizazi vijavyo.
0 Maoni:
Post a Comment