BAADHI YA MASHUHUDA WAKIWA KATIKA ENEO LA TUKIO
MZIGO ULIOKUA UMEBEBWA NA GARI AINA YA FUSO LIKELEKEA DAR ES SALAAM UKIWA PEMBEZONI MWA BARABARA
Ajali hiyo imetokea ikihusisha basi Mali kampuni ya ABOOD
ambalo liafanya safari zake kutoka Mbeya kwenda Dar Es Salaam ambalo lilifeli
breki katika mlima wa Kitonga uliopo wilayani Kilolo mkoani Iringa na kugonga
magari mawili na kisha kupinduka.
Basi hilo la abiria la Abood lenye namba za usajiri T729 AZG
Liligonga basi la kampuni ya HAPP NATION lenye namba za usajiri T427 DDT na
kisha kuligonga gari aina ya Fuso lenye nambari za usajiri T191 CXU Ambayo yote
yaliacha njia na kupinduka nje ya barabara.
Kamanda wa jeshi la Zima moto mkoani Iringa bwana Kennedy
Komba amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kua chanzo cha ajali ni
kufeli kwa breki kwa basi la Abood na kugonga basi la Happy Nation na Fuso
ambalo lilikua limebeba mzigo wa ndizi na yote yalikua yakielekea Dar Es
Salaam.
“Mpaka sasa majeruhi ni 12 na wengine wamepewa rufaa kutokana
na hali yao sio nzuri na kupelekwa Hospitali ya rufaa ya Mkoani Iringa”.
Alisema Komba
Komba amewataadharisha madereva kutokana na mlima huo hatari
kwa kuweka umakini wakati wanaendesha magari na kuendesha mwendo wa wastani
ambao hautaleta madhara katika jamii.
Aidha kamanda amesema wanampango mahsusi kuanzisha kituo cha
uokozi eneo la Ilula pindi tukio linapotokea waweze kutoa msaada kwa wakati.
Aidha ametoa rai kwa wananchi pindi matatizo ya ajali yanavyotokea waweze kutoa
taarifa kituo cha Polisi ili waweze kutoa msaada kwa haraka zaidi kwa kupiga
nambari ya Msaada ambayo ni bure 114.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mh Amina Masenza alifika eneo la tukio
na kujionea hali halisi ya ajali ilivyotokea na kusisitiza kwa madereva wote
wanaopita katika eneo hilo kua ni hatari na waweze kuchukua tahadhari kwani
tunazidi kupoteza maisha ya Watanzania.
Mbunge wa jimbo la Kilolo kupitia Chama Cha Mapinduzi Mh
Venance Mwamoto aliwahi kufika eneo la kituo akitokea katika ziara ya kikazi na
kupewa taarifa hizo kisha alikwenda eneo la Tukio na kutoa msaada kwa
kuwafikisha hospitali ya Ilula huku wengine waliokua na hali sio nzuri aliwapeleka
hospitali ya Rufaa ya Mkoani Iringa.
0 Maoni:
Post a Comment