Mwigizaji
na mrembo wa taji la Tanzania mwaka 2006 Wema Sepetu, amedai anapokea
vitisho vya kupotezwa kama ataendelea na msimamo wake wa kuitumikia
Chadema.
Wema
amesema yeye hatishwi na chochote, ameshaamua na hakuna mtu yeyote
atakaebadili mawazo yake kwa kuwa anachohitaji ni amani ya moyo wake na
kuwa huru kwani alikokuwa aliona nchi ilikuwa inaenda kubaya.
“Ninatishiwa sana, napigiwa simu na kutumiwa ujumbe mfupi wa maneno kwenye akaunti zangu na kwenye mitandao ya kijamii.
“Mimi
siogopi, nimeshaamua na hakuna wa kunizuia kwa hilo, kwani tangu
nimeingia katika chama hiki nina amani ya moyo na ninahisi nimetua mzigo
mzito niliokuwa nimeubeba,” amesema Wema.
Amedai
kuwa baadhi ya vitisho anavyopata ni matusi ya nguoni ambapo anaweza
kupigiwa simu na kutukanwa, wengine kumtumia ujumbe mfupi wakidai
watampoteza lakini anauhakika anayeweza kupoteza maisha yake ni Mungu.
Amesema
anajua amepata maadui ila anauhakika ni wachache sana kwani wengi
wanamuunga mkono na ukizingatia watu wake wa karibu wote wako naye bega
kwa bega hivyo hana sababu za kuogopa na anauhakika yuko kwenye chama
makini kinachojua nini maana ya demokrasia.
“Hakuna
mtu muhimu kama mzazi wako kama anakupa sapoti ya kutosha basi hakuna
mwingine atakayeweza kuzuia hilo, nashukuru wamejua nini ninakihitaji na
ninataka kuonyesha nini nilichokuwa nacho ambacho nilikokuwa
hawakukiona,” amesema Wema Sepetu.
Kwa
sasa Wema yuko katika ziara ya kutambulishwa mikoa yote kwa wanachama
na wapenzi wa Chadema na jana ameanzia Arusha kumtia moyo Mbunge wa
Arusha Mjini, Godbless Lema, anayekabiliwa na kesi ya uchochezi.
0 Maoni:
Post a Comment