MTENDAJI wa kijiji cha katili kata ya samazi wilaya ya
Kalambo mkoani Rukwa Oska Sauloni amejikuta kwenye wakati kwenye
wakati mgumu na kugeuza nyumba yake kuwa mahabusu ya
kuhifadhia watuhumiwa sambamba na kufanyia kazi za ofisi
nyumbani kwake kutokana na kijiji hicho kuwa na ukosefu wa
ofisi tangia nchi Tanzania kupata uhuru mwaka 1961
Kijiji cha katili kina jumla ya kaya 282 na wananchi 500
ambapo kati yao nguvu kazi ni wananchi 370 ambapo wananchi
wake wanajihusisha na shughuri za kilimo na uvuvi kupitia
ziwa Tanganyika.
Hata hivyo kijiji hicho kina ukosefu wa ofisi ya kijiji
, ambapo waharifu wanalazimika kufungiwa kwenye nyumba ya
mtendaji wa kijiji hicho na huku wengine wakilazimika kulala
na mtendaji kitanda kimoja kutokana na kijiji hicho kuwa
na ukosefu wa ofisi na mahabusu ndogo ya kuhifadhia
watuhumiwa ambao wamekuwa wakikamatwa na huku makao makuu
ya kituo cha polisi wilayani humo yakiwa zaidi ya umbali
wa km 30 kutoka kijiji husika.
Mtendaji wa kijiji hicho Osika sauloni ,amesema analazimika
kugeuka kuwa mgambo wa kijiji kwa kulala na watuhumiwa
kitanda kimoja nyumbani kwake ikiwemo kulazimika kufanyia kazi
za ofis nyumabani kwake kutokana na kijiji hicho kuwa na
ukofu wa ofis hali ambayo imekuwa ikimpa wakati mgumu
hususani nyakati za usiku pindi wtuhumiwa wanapo kuwa
wakileta fujo na kutaka kumpiga.
Mwenyekiti wa kijiji hicho ,Helmani Chitu ,ambae licha ya
kukili kuwep[o adha hiyo, licha hilo kijiji chake kina
kabiliwa na chanagamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa shule ya
msingi na zahanati na kusema kwa sasa wameanza ujenzi wa
shule ya msingi hivyo wakimaliza hilo ndipo wataanza kujenga
ofis na mahabusu.
Mtendaji wa kata hiyo Tedsoni Chonya amesema wananchi wameanza
kufyatua tofari kwa lengo la kukabiliana na chanagamoto hiyo.
Diwani wa kata hiyo Juma kibongwe amesema ametoa maagizo kwa
mwenyekiti wa kijiji hicho dhidi ya kuhamasisha wananchi
kujenga ofis ya mtendaji ili kuondokana na adha anazo
kabiliana nazo.
0 Maoni:
Post a Comment