Mnamo tarehe 05/03/2017 majira ya saa o5:30 usiku huko maeneo ya
Mafulala, kata ya Majengo, tarafa ya Lwiche, Manispaa ya Sumbawanga na
Mkoa wa Rukwa.
MKAZI mmoja wa Kata ya majengo mweye umri wa miaka 26, Malia
kokolo ,amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kuchomewa
nyumba yake na Joel Mwenga , Mwenye umri wa miaka 48, Mndali,
Mkazi wa Mafulala. Kutokana na wivu wa kimapenzi.
Kamanda wa polisi mkoani Rukwa Geoge Simba kyando amesema
Chanzo cha kufanya hivyo ni wivu wa mapenzi ambapo mlalamikaji alienda
kuulizia sababu za EMMANUEL MWENGA ambaye ni mtoto wa mtuhumiwa
kutangaza kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mlalamikaji.
Mbinu iliyotumika ni kwamba mtuhumiwa amekamatwa alimvizia mlalamikaji
akiwa amekimbia baada ya ugomvi kutokea ndipo akachoma nyumba.
Mtuhumiwa amekamatwa na atafikishwa mahakamani.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa Kamishna Msaidizi wa Polisi GEORGE
SIMBA KYANDO anatoa rai kwa wananchi kuacha kujichukulia sheria
mkononi na kuwashauri kupeleka migogoro yao sehemu husika ili waweze
kusaidiwa kuitatua kuliko kuchukua maamuzi magumu kama hayo.
Aidha anatoa onyo kwa wananchi kuwa makini kwani hatawafumbia macho
wale wote wanaofanya uhalifu.
0 Maoni:
Post a Comment