Mbunge wa viti maalumu CHADEMA Mkoa wa Iringa Mh Suzan Mgonokulima
Mh. Mbunge wa Viti maalumu Suzan Mgonokulima aliambatana na Baraza la Vijana CHADEMA (BAVICHA) Kwaajili ya kukabidhi msaada kwa wazee wa kijiji cha Migori kilichopo Wilayani Iringa Vijijini.
Mh. Mbunge alikwenda kutembelea Kata hiyo ya migori kuwatembelea wanawake wenzake wa kijiji hicho kutokana na siku ya maadhimisho ya siku ya wanawake kitaifa ambayo huadhimishwa kila mwaka mwezi March 8.
Wazee wakijiji hicho wameshukuru kupokea msaada huo kutoka kwa Mbunge pamoja na BAVICHA waliofika katika kijiji hicho.
0 Maoni:
Post a Comment