Mshauri mkuu wa baraza la usalama la taifa la Marekani, amerudishwa kwenye kazi yake ya awali baada ya kukosoa sera za utawala wa Donald Trump zinazohusiana na Latin America.
Msemaji wa Ikulu ya Marekani, Sarah Sanders, amesema Craig Deare ameondolewa kwenye nafasi hiyo. Deare alidaiwa kuponda jinsi uongozi wa Trump unavyoshughulika na masuala ya Latin America alipokuwa akizungumza huko Washington.
Hii si mara ya kwanza kiongozi wa juu anatumuliwa kwa kumkosoa Trump.
0 Maoni:
Post a Comment