Station mpya ya redio imetua jijini Dar es Salaam. Inapatikana kwenye masafa ya 103.3 (zamani yalikuwa yakitumiwa na BBC).
Kwa mujibu wa poster iliyowekwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga, station hiyo inaonekana kuwa ya muziki peke yake na tayari imepewa sifa za kuwa ‘Africa’s Number 1 Hits Station.’ Ni wazi kuwa inamilikiwa na kampuni hiyo ambayo hadi sasa ina redio mbili, Clouds FM na Choice FM. Bado haijajulikana itatumia jina gani.
Kwa sasa inapiga muziki peke yake.
0 Maoni:
Post a Comment