Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amesema anakubaliana na sera ya Rais wa Marekani Donald Trump kwamba “Marekani iwe ya Wamarekani”.
Bw Mugabe, ambaye ndiye mara ya kwanza anazungumzia utawala wa Bw Trump, amesema alishangazwa na ushindi wa kiongozi huyo wa Republican
.
Hata hivyo, amesema hakutaka pia “Madam Clinton ashinde”, akirejelea mgombea wa chama cha Democratic aliyeshindwa uchaguzi wa Novemba mwaka jana Hillary Clinton.
“Lakini vilevile, ukija kwa Donald Trump ambapo anazungumzia uzalendo, Marekani iwe ya Wamarekani – katika hilo, nakubaliana naye. Zimbabwe iwe ya Wazimbabwe,” Bw Mugabe amesema, kwenye dondoo ambazo zimechapishwa katika gazeti rasmi la serikali la Herald.
Ameongeza kwamba Bw Trump anafaa kupewa muda wa kudhihirisha uwezo wake.
“Sijui. Mpeni muda. Bw Trump huenda hata labda ataangalia upya vikwazo vilivyowekewa Zimbabwe,” Bw Mugabe amesema.
0 Maoni:
Post a Comment