Picha haihusiani na tukio husika
WANANCHI wa kijiji na kata ya Ikolo tarafa ya Unyakyusa wilayani Kyela mkoani Mbeya,wameikataa taarifa ya mapato na matumizi ya afisa mtendaji wa kijiji hicho,Danken Mwasipu wakidai kuwa inamapungufu lukuki huku wakimtuhumu kuuza viwanja vya kijiji kinyemela pasipo kuingiza fedha kwenye akaunti ya kijiji.
Wananchi hao,wamefanya mkutano mkuu wa kusomewa mapato na matumizi lakini ulivurugika baada ya afisa mtendaji na mwenyekiti wa kijiji kushindwa kutolea maelezo fedha za miradi ya kijiji walizokusanya.
Mwasipu anatuhumiwa kwa ubadhirifu wa fedha zitokanazo na mauzo ya lasilimali mbalimbali za kijiji ikiwemo miti ya mbao,ushuru wa bidhaa na ukodishwaji wa mashamba pamoja na kuchukua fedha kwa ajili ya kumilikisha ardhi pasipo mkutano mkuu.
Wananchi kijijini hapo wamekiambia kituo hiki kuwa afisa mtenda huyo amekuwa akipokea fedha za miladi ya kijiji na kufanyia kazi zake na huku mwenyekiti wa kijiji hicho akishindwa kuwajibika na kuwataka walejeshe fedha hizo.
Wamesema chanzo ni baada ya siku za hivi karibuni mtendaji huyo alipewa fedha kias cha shilling laki nane 800000/= ili azipeleke benki lakini cha kusikitisha fedha hizo hazikupelekwa benki na huku kila wakihoji wamekuwa wakipigwa dana dana kama mpira wa kona na kuona kama wanahujumiwa kimachomacho.
Kwa upande wake afisa mtendaji wa kijiji hicho,Danken Mwasipu,amesema ni kweli alipokea fedha hizo za umilikishaji ardhi lakini alishindwa kuiingiza kwenye kijiji kutokana na kuwa na migogoro ya mipaka na kuwa endapo wale waliotoa fedha hizo wakizihitaji wafike ofisini kwake atawarejeshea.
Mwenyekiti wa kijiji hicho,Bonifasi Mwakilema licha ya kukiri kuwepo kwa tuhuma hizo,amesema ndiyo maana wanafanya mikutano ili kila kitu kiwe wazi na kuwa anawaomba wanakijiji kupitia mkutano waipokee taarifa hiyo ili mambo mengine yafuate,kitu ambacho kilipingwa vikali na wananchi hao.
Diwani wa kata hiyo,Angomwile Mumbimbe,amekili kuwepo na tuhuma hizo na kudai kuwa aliwaeleza wananchi kuwa wafuate taratibu za madai yao pasipo kuvunja amani iliyopo na kuhusu ujenzi wa vyoo amesema ujenzi uendelee pesa zitolewe na Mtendaji na ikionekana umekwama atabeba lawama zote.
Mpaka kikao hicho kinavunjika,wananchi waliikataa taarifa hiyo wakihitaji fedha zote ziingizwe kwenye akaunti ya kijiji kabla ya kuendelea na ajenda zingine na kusema kuwa wiki ijayo wataenda ofisini kwa mkuu wa wilaya ili aweze kuingilia kati suala hilo.
0 Maoni:
Post a Comment