Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
amewaagiza majaji na mahakimu wanawake kote nchini kupambana ipasavyo
katika kukabiliana vitendo vya rushwa,unyanyasaji kijinsia na rushwa ya
ngono ili kusaidia wanawake kupata haki zao za msingi bila kubaguliwa
katika jamii.
Makamu
wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa agizo hilo jijini Dar es Salaam
wakati anafungua Mkutano Mkuu wa NANE wa Chama cha Majaji na Mahakimu
wanawake Tanzania (TAWJA).
Makamu
wa Rais pia ameonya kuhusu vitendo vya rushwa ya ngono inayofanywa na
baadhi ya watendaji wenye madaraka na kusema tabia hiyo ni mbaya na
lazima ikomeshwa mara moja katika jamii.
Amesema
kuwa vitendo hivyo vya rushwa ya ngono huzuia na kukwamisha juhudi za
wanawake kufikia huduma za kijamii na za kiserikali ipasavyo ikiwemo
elimu, ajira na haki kwa ajili ya ustawi wa wanawake.
Aidha
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amekishukuru Chama cha Dunia cha
Majaji Wanawake (IAWJ) kwa mchango na msaada wake kwa TAWJA katika
programu ya miaka mitatu ya kupambana na matumizi mabaya ya madaraka na
rushwa ya ngono.
Makamu
wa Rais pia ameipongeza Wizara ya Katiba na Sheria, Shirika la UN Women
na wadau wengine wa TAWJA kwa kuunga mkono mapambano ya aina zote za
ubaguzi na ukatili dhidi ya wanawake na watoto nchini.
Amesema
elimu ya haki za Binadamu iliyotolewa na Chama hicho imeleta badiliko
kwa wengi kwa njia ya mafunzo na machapisho na jitihada hivyo lazima
ziongezwe ili huduma hiyo iweze kuwafikia wananchi wengi zaidi kote
nchini.
Amesisitiza
wanachama wa Chama cha TAWJA waendelee kutoa msaada katika kuwasaidia
wanawake na watoto ambao wanakandamizwa kwa kunyimwa haki zao katika
jamii ili waweze kupata haki zao nchini.
Kwa
upande wake, Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mohamed
Chande Othman amemhakikishia Makamu wa Rais kuwa mkakati wa uimarishaji
wa shughuli za mahakama nchini unaendelea vyema lengo likiwa ni kutenda
haki kwa wananchi kote nchini bila ubaguzi.
Kauli
mbiu ya Mkutano Mkuu wa NANE wa Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania
(TAWJA) “Kuongoza njia kufikia hitajio la upatikanaji wa haki kwa wote
na kwa wakati”.
Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
Dar es Salaam
7-Jan-2017.
0 Maoni:
Post a Comment