Rais wa Cuba, Raul Castro aliongoza tukio la kutolewa heshima za mwisho kwa kaka yake, Fidel kwenye jiji la Santiago.
Makumi kwa maelfu ya wananchi wa Cuba walihudhuria sherehe hizo pamoja na viongozi wa dunia.
Raul Castro aliapa kuenzi misingi ya kisocialist iliyowekwa na mwana mapinduzi huyo aliyefariki dunia November 25 akiwa na miaka 90. Alitangaza pia kuwa Cuba itapiga marufuku majengo au barabara kupewa jina la Fidel Castro, kutokana na ombi la kiongozi huyo.
Pia alisema hakuna sanamu ya Fidel itakayowekwa Cuba. Viongozi wa Venezuela, Nicaragua na Bolivia walihudhuria hafla hizo.
0 Maoni:
Post a Comment