Mwenyekiti wa Taifa wa Bodi ya Parole,Dkt. Augustine Mrema akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo Novemba 17.2016, Jijini Dar es Salaam.(Picha na Andrew Chale)
Mwenyekiti wa Taifa wa Bodi ya Parole, Dkt. Augustine Mrema amemwandikia barua Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Kassim Majaliwa kulalamikia jeshi la Magereza kukwamisha mpango wake wa kuwatoa wafungwa ambao tayari wameshalipiwa fedha na wasamalia wema baada ya kukidhi vigezo.
Dkt. Mrema ameyasema hayo mchana huu wakati wa
kutoa taarifa yake hiyo kwa waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam
kuzungumzia suala lake hilo la Maafisa wa Magereza kusitisha hatua ya kukatisha
mpango wake licha ya kuwalipia wafungwa waliokidhi vigezo.
“Mimi nimeona nisinyamaze. Napaza sauti nataka
Rais aone, ajue kama magereza yetu yanashida na tunalotatizo kwa nini mpango
huu umesimamishwa na umesitishwa tumekosea wapi?. Nimesha muandikia barua
Waziri Mkuu kulalamikia jeshi la Magereza kukwamisha mpango huu na watu 43
tayari tumesha walipia faini hiyo lakini bado wapo magerezani wanasota. Mrema
amefanya kosa lipi? Ama Mama Mchungaji Getrude Rwakatare amekosa nini? Mpaka
wamesitisha zoezi hili” amesema Mrema kwa waandishi wa habari.
0 Maoni:
Post a Comment