Mgombea wa nafasi ya urais kupitia Chama cha Democratic, Hillary Clinton katika uchaguzi wa Marekani uliofanyika wiki iliyopita ameeleza masikitiko yake kwa kushindwa na Donald Trump katika uchaguzi huo.
Clinton amesema kuwa baada ya matokeo ya kushindwa na Trump hakutaka kuwa akitoka hata nyumbani na anapenda kwa sasa muda mwingi kuwa nyumbani akijishughulisha mambo mengine tofauti na siasa.
“Nimekubali kuja hapa usiku wa leo lakini halikuwa jambo rahisi kwangu,” alisema Clinton na kuongeza.
“Imekuwa ni mara chache na tangu wiki iliyopita ninachotaka kufanya muda wote ni kufanya mazoezi ya viungo na kusoma vitabu vizuri na sihitaji kuondoka tena nyumbani”
Jambo hilo kwa Clinton yawezekana linasababishwa na matarajio makubwa ya kushinda uchaguzi aliyokuwanayo kutokana na kura za maoni kuonyesha kuwa Clinton angemshinda Trump kwa sababu alionekana kukubalika na watu wengi lakini baada ya uchaguzi kufanyika Trump akaibuka mshindi.