Hivi karibuni kumekuwa na taarifa zilizosambaa katika mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari zinazodai kuwa uongozi wa Simba umekuwa ukichelewa kuwalipa mishahara wachezaji wake kwa miezi miwili.
Kupitia ukurasa wa instagram wa klabu ya Simba Sc Tanzania Katibu mkuu wa Simba, Patrick Kahemele amezungumzia juu ya upotovu wa taarifa hizo na kusema kuwa hakuna ukweli wowote juu ya taarifa hizo “Wachezaji wa Simba wanalipwa mishahara, inaweza kuchelewa kwa wiki moja au wiki mbili ni jambo la kawaida, ni process kwasababu unapokuwa unachukua pesa kutoka kampuni nyingine hadi iwe transferred kwenye akaunti zako it take time, lakini pia hapa katikati tulipata tatizo baada ya mashabiki wetu kuvunja viti kwenye mchezo na watani wetu wa oktoba mosi, kuna fedha za mechi ile zilikuwa held mpaka leo hazijatoka kwahiyo cash flow ikayumba lakini haimaanishi wachezaji hawalipwi,” alisema Kahemele.
Aidha pia aliongezea Kuhusu swala la mikataba ya wachezaji inayokaribia kuisha na kusema kuwa inafanyiwa kazi na imepewa uzito mkubwa unaostahili.
Kahemele alitoa rai kwa wapenzi wa Simba kutowapa nafasi watu wachochezi wanaotoa taarifa za uongo na kuto amini juu ya minong‘ono yenye lengo la kuitoa timu kwenye mchezo.
0 Maoni:
Post a Comment