Beki wa klabu ya Yanga, Andrew Vincent 'Dante' jana alipewa mikoba ya kuwa kapteni wa timu hiyo kufuatia kutokuwepo kwa Kelvin Yondani pamoja na Nahodha Mkuu, Nadir Haroub 'Cannavaro'.
Dante amefanikiwa kupata fursa ya kupata majukumu hayo ya Ukapteni wa muda, ikiwa ni katika mchezo kimataifa wa kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya U.S.M Alger ambao ni wa kwanza kwake.
Nafasi hiyo hutumiwa mara nyingi na Kelvin Yondani kama msaidizi inapotokea Nahodha mkuu, Cannavaro hajaanza.
Baada ya mchezo huo kumalizika jana, Yanga inatarajiwa kuwasili nchini kesho ambapo imeanza safari ya kurejea Dar es Salaam leo.
0 Maoni:
Post a Comment