WAZAMBIA WATUA NCHINI KUIKABILI TWIGA STARS

Kikosi cha timu ya taifa ya wanawake kutoka Zambia kimewasili jijini Dar es Salaam tayari kwa mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wanawake dhidi ya Twiga Stars.
 
Kikosi hicho cha Zambia kitacheza na Twiga Jumatano ya wiki hii katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ikiwa ni mechi ya kwanza katika kuwania tiketi ya kufuzu AFCON 2019.
 
Hata hivyo, baada ya mechi hiyo ya kwanza Twiga Stars itasafiri kuelekea Zambia kwaajili ya mchezo wa marudiano utakaofanyika baada ya wiki mbili.
Share on Google Plus
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment