Majambazi wamevamia Parokia ya Mtakatifu Teresia, Mbezi Mwisho jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo na kupora sadaka na vikombe vitano vya misa, usiku wa kuamkia leo.
Kwa mujibu wa Padre wa Dekano ya Kibaha ya Kanisa Katoliki, Fr Benno Kikudo, walinzi wa Parokia walipigwa na kuumizwa ila hawakuweza kuifikia nyumba ya mapadre. “Usiku wa kuamkia leo, mapadre wenzetu wa parokia ya Mt Teresia, Mbezi Mwisho waliingiliwa na majambazi kanisani.
Majambazi walivunja mlango wa sakristia. Wameiba sadaka na vikombe vitano vya misa. Majambazi waliwapiga na kuwaumiza walinzi wa parokia. Bahati nzuri hawakuingia nyumba ya mapadre,” ameandika Fr Kikudo. “Baba Paroko Fr Sunnil amenipatia taarifa asubuhi hii. Tumpatie pole Baba Paroko na mapadre wote pole,” ameongeza katika taarifa yake
0 Maoni:
Post a Comment