Mabingwa wa soka Tanzania bara Young Africans wamepangwa kupambana na Welayta Dicha ya Ethiopia katika mchezo wa kuwania kufuzu hatua ya makundi ya kombe la shirikisho barani Afrika.
Young Africans wamepangwa kukutana na klabu hiyo, baada ya kuondolewa kwenye michuano ya klabu bingwa barani Afrika mwishoni mwa juma lililopita.
Young Africans iliondolewa ligi ya mabingwa kwa jumla ya mabao mawili kwa moja dhidi ya Township Rollers ya nchini Botswana.
Welayta Dicha walifanikiwa kuendelea katika michuano ya kombe la shirikisho kwa kuwaondoa mabingwa wa zamani wa Afrika Zamalek FC kwa changamoto ya mikwaju ya penati mwishoni mwa juma lililopita.
Katika mchezo wa mkondo wa kwanza Welayta Dicha waliifunga Zamalek mabao mawili kwa moja, kabla ya matokeo kama hayo kuwageukia wakiwa ugenini.
Katika changamoto za mikwaju ya penati Welayta Dicha waliibuka kidedea kwa mikwaju minne kwa mitatu.
Michezo mingine ya kuwani kutinga hatua ya makundi ya kombe la shirikkisho.
Zanaco v Raja Casablanca
AS Vita v CS La Mancha Brazaville Kongo
St George v CARA Brazzaville (DRC)
El Hilal v Akwa United
SuperSport United v Gor Mahia
Al-Hilal Al-Ubayyid v UD Songo
USM Alger v Plateau United
Enyimba v Bidvest Wits
Aduana Stars v Fosa Juniors
Young Africans v Welayta Dicha
Génération Foot v RS Berkane
CF Mounana v Al-Masry
ASEC Mimosas v CR Belouizdad
Williamsville AC v Deportivo Niefang
MFM v Djoliba
Rayon Sports v Costa do Sol
AS Vita v CS La Mancha Brazaville Kongo
St George v CARA Brazzaville (DRC)
El Hilal v Akwa United
SuperSport United v Gor Mahia
Al-Hilal Al-Ubayyid v UD Songo
USM Alger v Plateau United
Enyimba v Bidvest Wits
Aduana Stars v Fosa Juniors
Young Africans v Welayta Dicha
Génération Foot v RS Berkane
CF Mounana v Al-Masry
ASEC Mimosas v CR Belouizdad
Williamsville AC v Deportivo Niefang
MFM v Djoliba
Rayon Sports v Costa do Sol
0 Maoni:
Post a Comment