NONDO SASA HURU KWA DHAMANA


Mahakama ya hakimu Mkazi Mkoa wa Iringa imemuachia  huru kwa dhamana Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania(TSNP), Abdul Nondo.

Mahakama imemwachia baada ya kutimiza Masharti mawili ambayo ni kuwa na Wadhamini wawili wakazi wa Iringa na mmoja lazima awe Mtumishi wa Serikali ambapo Wote kwa pamoja wamesaini bondi ya kauli Shilingi Milioni 5.

Hakimu mkazi mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Iringa, John Mpitanjia amesema Baada ya kuachiwa kwa dhamana Abdul Nondo Kesi yake itatajwa tena Aprili 10, 2018. 

Nondo anatuhumiwa kwa makosa mawili ambapo Kosa la kwanza ni kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni Machi 7, 2018 akiwa Ubungo na kusambaza kwa kutumia mtandao wa WhatsApp kuwa yupo hatarini.

Shtaka la pili ni kutoa taarifa za uongo kwa watumishi wa umma mjini Mafinga alipokuwa akitoa taarifa katika kituo cha Polisi Mafinga kuwa alitekwa na watu wasiojulikana jijini Dar es Salaam na kupelekwa Kiwanda cha Pareto cha Mafinga.
Share on Google Plus
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment