MWANAFUNZI WA UDSM ALIYETOWEKA AMEPATIKANA MAFINGA IRINGA

Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania , Abdul Nondo ambaye pia ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) aliyeripotiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha amepatikana akiwa hai eneo la Mafinga mkoani Iringa.

Imeelezwa kuwa, Nondo alijikuta katika eneo hilo baada ya kuzinduka kutoka katika lindi la usingizi na kuwauliza wenyeji wa eneo hilo kuwa hapo ni wapi? Wenyeji hao walimfahamisha kuwa yuko Mafinga mkoani Iringa na kisha akapelekwa katika kituo cha polisi kilichoko karibu.

Polisi walifanya mahojiano na mwanafunzi huyo ili kuweza kujua nini hasa kilitoka na baada ya hapo kupiga simu kwa ndugu zake.

Baada ya Baba mzazi, Mussa Mitumba kupata taarifa za kuonekana kwa mwanae, aliomba namba za askari aliyemfanyia mahojiano ili kujua nini kilimpata mwanae aweze kujua kama jambo jingine alilowaambia kuhusiana na kupotea kwake.

Awali kabla ya tukio hilo mwanafunzi huyo alielezea kwamba alikuwa akifuatiliwa mara kadhaa watu asiowatambua na wenye nguo za kiraia wakijitambulisha kama watu wa usalama ambao wamekuwa wakimpatia vitisho.
Share on Google Plus
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment