AJINYONGA BAADA YA KUTUHUMIWA KUIBA BATA

 
MWANAMKE Costansia Kadogo James (37), mkazi wa kijiji na kata ya Kisorya, tarafa ya Nansimo wilaya ya Bunda mkoani Mara, amejinyonga hadi kufa kwa kutumia kamba.

Mama huyo alijinyonga baada ya kutuhumiwa kuiba bata mmoja, mali ya jirani yake na kusababisha vifaranga vinne kati ya saba vya bata huyo kufa na kutakiwa wazazi wake wamlipe fidia mwenye bata.

Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kisorya, Revocatus Luheneja, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo juzi katika kijiji cha Kisorya kati ya saa kumi na 11:00 jioni. Alisema kuwa mwanamke huyo alijinyonga kwa kamba baada ya kuiba bata wa jirani yake aitwaye Venaida Charles, mkazi wa kijiji hicho na kwenda kumuuza kwa mwananchi mmoja anayetambulika kwa jina la Mkanga Mchomanyama.

Ofisa Mtendaji huyo alisema kuwa baada ya mwenye bata kukuta bata wake ameibwa, huku akiwa ameacha vifaranga vitatu na vinne vikiwa tayari vimekwisha kufa, alifuatilia na ndipo alipomkuta kwa mwananchi huyo aliyedai ameuziwa na mwanamke huyo ambaye kwa sasa ni marehemu.

Alisema kuwa akiwa na wananchi wengine alichukuwa vifaranga hivyo vilivyokuwa vimekwisha kufa na bata wake na kwenda navyo kwa wazazi wa mwanamke huyo kwa ajili ya kudai fidia.

Ofisa Tarafa ya Nansimo, Jonas Nyaoja alisema kuwa tayari tukio hilo limeripotiwa kituo kidogo cha polisi Kisorya, ambapo wanamshikilia mwanamke aliyeibiwa bata wake kwa uchunguzi zaidi, ikiwa ni pamoja na kuisaidia polisi. Maofisa wa polisi wilayani hapa, ambao hawakuwa tayari kutaja majina yao kwa madai kwamba wao siyo wasemaji wa jeshi hilo waliozungumza na gazeti hili walithibitisha kuwepo kwa tukio hilo.
Share on Google Plus
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment