Ligi Kuu Uingereza inaendelea tena leo kwa mechi moja kuchezwa Emirates Stadium ambapo Arsenal itakuwa inaikaribisha manchester City.
Arsenal iliyotoka kujeruhiwa na Manchester City kwa mabao 3-0 katika fainali ya Carabao Cup na kumpa Guardiola taji la kwanza, inajipanga kulipiza kisasi leo
Kuelekea mchezo huo, Kocha Wenger amesema walisikitishwa na matokeo ya mechi iliyopita baada ya kufungwa 3-0, hivyo kwa sasa akili yao yote wanaiweka kwenye mchezo wa leo ili wapate matokeo.
Kwa upande wa Pep Guardiola, naye amesema siku zote anapokutana na arsenal mchezo huwa mgumu, yawezekana wakawa hawapo vizuri msimu huu lakini mechi itakuwa ngumu.
0 Maoni:
Post a Comment