Jeshi
la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limemkabidhi mfanyabiashara
Yusuf Manji na wenzake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya
kumaliza kumuhoji katika kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili.
Wakili
wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi amemueleza Hakimu Mkazi
Mkuu, Huruma Shaidi kuwa washtakiwa hao wamerudishwa kama Mahakama
ilivyoamuru warudishwe baada ya Polisi kumaliza kuwahoji.
Baada
ya kusema hayo, Hakimu Shaidi alisema kesi hiyo itaendelea na utaratibu
kama ilivyo awali, ambapo ameahirisha hadi September 8, 2017.
Awali
Mahakama hiyo iliruhusu Yusuf Manji na wenzake watatu kwenda kuhojiwa
na Polisi kwa lengo la kukamilisha upelelezi wa kesi ya uhujumu uchumi
wanayokabiliwa nayo.
Mbali
na Yusuf Manji, washitakiwa wengine waliokabidhiwa ni Meneja Rasilimali
watu wa Kampuni ya Quality Group Ltd, Deogratius Kisinda, Mtunza Stoo,
Abdallah Sangey na Thobias Fwere.
0 Maoni:
Post a Comment