YANGA ‘KUTESTI MITAMBO’ TENA JUMAMOSI NA JUMAPILI DAR NA ZENJI

 Young Africans SC (logo).png
MABINGWA wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga SC watacheza mechi mbili mfululizo za kujipima nguvu Jumamosi na Jumapili kujiandaa na msimu mpya.
  Jumamosi Yanga watamenyana na Ruvu Shooting Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kabla ya Jumapili kuwafuata Mlandege Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
  Yanga SC inatarajiwa kuondoka Dar es Salaam Jumapili asubuhi kwenda Zanzibar kuweka kambi ya kujiandaa na mchezo dhidi ya mahasimu, Simba SC wiki ijayo.  
  Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga imesema kwamba timu inaendelea na mazoezi Dar es Salaam kujiandaa na mechi hizo.

Michezo hiyo inafuatia wa Jumamosi iliyopita, Yanga ilipotoka nyuma kwa mabao 2-1 na kushinda 3-2 dhidi ya Singida United Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, winga Emmamuel Martin akifunga la ushindi dakika ya mwisho.  
 
Lakini Jumamosi Yanga watacheza kwa mara kwanza baada ya Yanga kukamilisha usajili wao wa msimu mpya- maana yake huo ndio mchezo ambao mashabiki wa timu hiyo watapata fursa ya kukijua rasmi kikosi chao kamili cha msimu mpya.

 
Kwa kocha Mzambia, George Lwandamina hiyo itakuwa michezo ya kukipima kikosi chake kwa mara ya mwisho kabla ya kuingia kwenye mchezo na wa Ngao ya Jamii dhidi ya mahasimu, Simba Agosti 23 Uwanja wa Taifa.

 
Bila shaka Jumamosi wana Yanga watapata fursa ya kumuona kwa mara ya kwanza kiungo Mkongo, Papy Kabamba Tshishimbi akiichezea timu yao baada ya kusajiliwa kutoka Mbabane Swallows ya Swaziland. 

Share on Google Plus
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment