Vigogo Escrow, IPTL waongezewa mashitaka mapya 6

Jamhuri imeongeza mashitaka mapya sita kwa watuhumiwa wa kesi ya Escrow na IPTL, James Rugemalila na Habinder Seth Sigh, na kufanya idadi ya mashitaka yanayowakabili vigogo hao kufikia 12.

Leo Julai 3, 2017, Mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Huruma Shahidi, Wakili upande wa Jamhuri, Shadrack Kimaro aliwasomea Mashtaka Mapya watuhumiwa hao ikiwemo uhujumu uchumi, kula njama, kughushi pamoja na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kuisababishia serikali hasara.

Awali watuhumiwa walishtakiwa kwa mashtaka sita na sasa yameongezwa sita mengine na kufikia 12.
Aidha, kesi hiyo imepangwa kutajwa tena Tarehe 14 Julai 2017.
Share on Google Plus
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment