Miezi
kadhaa iliyopita mwanamke mmoja aliyejitambulisha kwa jina la
Thoeflida wa Yesu,alisambaza waraka kwenye vyombo mbalimbali vya
habari nchini Tanzania na Kenya, akieleza kuwa alimteka
kimapenzi mume wa mtu kwa kutumia uchawi wa limbwata la nyama
ya bundi wa kichawi . Katika waraka wake huo mwanamke huyo
anadai aliupata uchawi huo kutoka kwangu mimi Dokta MUNGWA
KABILI.
Baada
ya kusambaa kwa waraka huo, nimekuwa nikipokea simu kutoka kwa
waandishi kutoka sehemu mbalimbali pamoja na watu mbalimbali
wakiniomba nitoe ufafanuzi kuhusu waraka huo.
Ili
kuondoa usumbufu wa kuulizwa maswali yale yale kila wakati,
nimeamua kuandika waraka wa ufafanuzi kuhusu makala ya
mwanadada huyo.
Lakini
kabla sijaanza kutolea ufafanuzi kuhusu waraka huo, ni vyema
nikauweka hapa waraka huo ili nitakapo anza kutoa majibu ya
ufafanuzi kuhusu waraka huo, kusiwe na maswali mengine yasiyo
na msingi.
USHUHUDA WA THEOFLIDA WA YESU : NILIMLISHA MUME WA MTU, LIMBWATA LA NYAMA YA BUNDI.
Nawasalimu
wa jina la YESU, jina kuu kupita majina yote. Jina langu
ninaitwa Theoflida , ni mwanamke mwenye umri wa miaka 38 mkaazi
wa Mbezi ya Kimara jijini Dar Es Salaam, japo kiasili ni
mwenyeji wa wilaya ya Ulanga, mkoani Morogoro..
Nime
amua kuandika waraka huu kwa madhumuni makuu mawili, kwanza ni
kushuhudia MATENDO MAKUU ambayo YESU AMENITENDEA na pili, ni
kuwa hasa wanawake wenzangu kutojihusisha kabisa na masuala ya
WAGANGA WA KIENYEJI kwa sababu waganga wa kienyeji ni MAWAKALA
WA KAZI ZA SHETANI HAPA DUNIANI na ni MASHETANI KABISA!...
Nitaanza kwa kuelezea kisa kilicho nipelekea kuingia kichwa kichwa kwenye mikono ya wakala wa shetani..
Nilikuwa
nimepanga chumba kimoja maeneo ya Tabata Mawenzi huku
nikijihusisha na biashara ya genge. Jirani na nyumba niliyokuwa
nimepanga, aliishi mwanaume mmoja na mke wake. Mwanaume huyu
jina lake linaanzia na herufi K hivyo katika maelezo yangu
nitakuwa nikimtaja kwa herufi K.
K
alikuwa ni mwanaume mwenye mafanikio makubwa katika maisha
mwenye kazi nzuri. Alikuwa na nyumba zaidi ya moja, magari ya
kifahari. viwanja , mashamba, na miradi mbalimbali iliyokuwa
ikimlipa vizuri sana. Kwa ufupi K alikuwa tajiri mwenye maisha
mazuri.
K
na mke wake wote walikuwa wenyeji wa wilaya ya Muleba,mkoani
Kagera . Ndoa ya K na mkewe ilikuwa na umri wa mwaka mmoja...
K
na mke wake waliishi maisha mazuri sana....Kwa sababu ya
ugumu wa maisha yangu, nikajikuta naanza kutamani maisha ya mke
wa K.. Nikawa natamani mimi ndo ningekuwa mke wa K na
kufurahia maisha vile mke wa K alivyo kuwa akifurahia.
Nilimuona mke wa K kama mtu mwenye bahati sana na kutamani
bahati hiyo iwe yangu.
Baada
ya wazo hili kukomaa ndani ya nafsi yangu, nikaanza kutafuta
njia ya kumteka K kimapenzi na kuchukua nafasi ya mke wake.
Njia pekee niliyo ona inafaa, ni kutumia uchawi.
Sasa
basi, kuna rafiki yangu mmoja, anaitwa Pamela. Pamela alikuwa
anapenda sana mambo ya waganga waganga, kwa hivyo alikuwa
anawajua waganga wengi. Hata katika biashara yangu ya genge,
alishanipeleka kwa waganga kadhaa kwa ajili ya kupata dawa ya
mvuto wa bishara yangu..
Nilipo
mfuata Pamela, akaniambia kuna mganga mmoja, ni mkali sana wa
mambo ya mapenzi.. Mi mwenyewe nina mpango wa kumtafuta lakini
najipanga kwanza kwa sababu bei zake ni kubwa.
Pamela
akasema alimfahamu mganga huyo alipokuwa katika kijiji cha
Mwalusembe, wilayani Mkuranga.. Siku hiyo kuna fumanizi lilitokea,
mwanaume alikuwa anatembea na mke wa mtu, kumbe huyo mwanamke
alikuwa amewekewa tego, huyo mwanaume alipo muingilia mwanamke
huyo, wakawa wamenasana.. Baadae ikatafutwa namba ya simu ya mume
wa mwanamke. Mume alipofika kufumania, akakuta mke wake
amenasana na mgoni wake.. Akaitwa huyo Mganga kwa sababu ndie
aliye weka hilo tego, alipofika eneo la tukio alifanya uganga
wake, wale wagoni wakawa wameachana.. Tukio hilo lilivuta watu
wengi sana.. Kwa hiyo Pamela anasema, alimjulia mganga huyu
kwenye tukio hilo... Akafanikiwa kutafuta na kupata namba zake.
Pamela
akanipa namba za simu za mganga huyo, nilivyo mpiugia akasema
yupo Handeni kikazi ila baada ya siku tatu atakuwa Bagamoyo
ambapo atakaa hapo kwa mwezi mzima aki agua watu wenye
matatizo mbalimbali.
Kweli
baada ya siku ya tatu, nikaenda hadi Bagamoyo kuonana na
huyo mganga ambaye jina lake tu ni kufuru kubwa kwa Mungu.,.
Yeye anajiita MUNGU WA KABILI ambayo tafsiri yake ni MUNGU WA
PILI. Lakini pia nilishangaa kumuona mganga mwenyewe anaokena
bado kijana ambaye sidhani kama ana fikisha miaka arobaini.
NAANZA KWA KUPIMWA MWILI WANGU KICHAWI
Mungu
wa Kabili akasema kabla, hajaanza kazi ya ‘kumtengeneza’ K ,
inabidi aanze kwanza kuuangalia mwili wangu ili ajue kama ni
msafi ama mchafu.
Basi
nikapewa dawa nimeze, halafu nikaambiwa Yule kuku mweusi ambaye
nilienda nae mwenyewe, nimshike kichwani. Baada ya hapo, Dokta
Mungu wa Kabili akaanza kuongea maneno yake ya kiganga huku
akiwa ameshikilia chungu chenye dawa iliyo katika mfumo wa
maji maji.. Alifanya hivyo kwa muda wa kama dakika kumi na
tano hivi. Alipomaliza kufanya uganga wake, akaniambia nimtue
Yule kuku mweusi niliekuwa nimembeba kichwani. Nilipo mtua
nikashangaa kumuona kuku Yule amekufa. Niliogopa sana .
Basi
Mungu wa Kabili, akaniambia mwili wangu ni mchafu sana. Roho
ya mauti imepandwa kwenye mwili wangu. Hivyo lazima anisafishe
kwanza, kutoa uchafu ulio pandikizwa mwilini wangu kichawi. Baada
ya hapo ndio tutaendelea na zoezi la kumfanyia ulozi K.
Mungu
wa Kabili akaniambia niende nyumbani, nirudi siku inayo fuata
jioni ya saa kumi na mbili nikiwa na sarafu 350 za shilingi
mia mbili mbili ambazo jumla yake ni Shilingi Elfu Sabini,
mchanga wa njia panda saba, pamoja na wembe tatu..
NASAFISHWA MWILI WANGU KICHAWI.
Ilipo
fika saa sita kamili za usiku, mimi , Dokta Mungu Wa Kabili
pamoja na msaidizi wake, tukaongozona hadi njia panda. Njia panda
hiyo ipo huko huko Bagamoyo porini..
Tulibeba,
kigoda, chungu , vifaa nilivyo kuja navyo ( mchanga, wa njia panda
saba, sarafu 350, pamoja na asali nusu lita ), mawe matatu,
mishumaa ya rangi nyekundu, mkaa, pamoja na dawa nyingine
zilizokuwa kwenye vibuyu kama saba hivi.
Tulipofika
eneo la njia panda, Mungu wa Kabili, alizungushia dawa
kuzunguka eneo tulipoweka vitu vyetu, akamuagiza msaidizi wake,
awashe mishumaa ambayo idadi yake ilikuwa kumi na nne, mishumaa
hiyo iliwekwa kuzunguka eneo tulilokuwa sisi. Baada ya hapo,
ukawasha moto, kwenye mafiga kisha chungu kikatengwa pale,
nikaweka vitu vyangu vyote nilivyo kuja navyo, na yeye Mungu
wa Kabili, akachanganya dawa zake anazo zijua mwenyewe…
Baada
ya kama dakika arobaini hivi, zile dawa zikawa zimecheka,
nikapewa kibuyu nikaambiwa nikoge kwa kuchota maji ya kwenye
chungu huku chungu kikiwa kinachemka. Nikafanya kama nilivyo
elekezwa huku mganga akiwa anaongea vitu vyake vya kiganga
ambavyo sikuweza kuvielewa..
Nilipomaliza
kuoga, mganga akanichanja karibu mwili mzima, kisha nikapakwa
hiyo asali. Baada ya hapo, tukarejea kilingeni . Mungu wa Kabili
akaniambia nipumzike, ikifika saa kumi na moja alfajiri niamke
kwa ajili ya kupikwa. Akasema zoezi la kwanza lilikuwa
kunisafisha na kuniosha kwanza, ambalo limeshakamilika, kinacho
fuatia ni kupikwa.
NAPIKWA KICHAWI…
Ilipofika
alfajiri nilidamka, kama nilivyo agizwa na mganga kwa ajili ya
zoezi la kupikwa kichawi.. Nikaelekezwa kuingia katika chumba
maalumu ambako kulikuwa na chungu kikubwa. Ndani ya chungu
hicho yaliwekwa maji ya baharini, majani ya mti unaitwa muosha
fedha ama mfedha mfedha, majani ya mkaratusi pamoja na majani
ya mti unaitwa mkuyu, halafu ndani yake zikawekwa sarafu
zilizoisha kutumika muda wake, pamoja na dawa nyingine kama
tano hivi ambazo sikuambiwa ni dawa gani…
Baada
ya hapo, nikaambiwa nikatwe nywele zangu, pamoja na kucha zangu.
Baada ya kukatwa nywele zangu, vitu vyote hivyo vikachukuliwa
vikafungwa kwenye kitambaa chekundu, ndani ya kitambaa hicho
zikaongezwa dawa nyingine , halafu vikawekwa kwenye chungu kwa
ajili ya kupikwa.
Katika
chungu hicho pia vikawekwa visu saba, vikiwa vimesimama. Baada
ya kama dakika kumi na tano hivi, mganga akamwambia msaidizi
wake, ‘ hebu ongeza chumvi humo ‘. Nikatarajia kuona itakuwa
chumvi ya kawaida ninayo ijua mimi, ila nikashangaa kuona
kinawekwa kipande cha mti..
Baadae
nilikuja kugundua kuwa, katika uganga na uchawi kuna kitu
kinaitwa ‘Chumvi ya Kichawi” kazi ya chumvi ya kichawi ni
kuukoleza uchawi ama kukoleza nguvu ya dawa.
Mganga
aliniambia vitu vyangu yaani nywele pamoja na kucha
vinaniwakilisha mimi, kwa hiyo kupikwa kwa vitu vyangu
kunamaanisha mimi ndio nimepikwa. Baada ya dawa kupikwa,
nikapewa maji yale na kuelekezwa kwenda kuoga. Nikaambiwa
nikimaliza kuoga niende nikapumzike kwenye chumba change hadi
nitakapo pewa maelekezo mengine.
NAFANYIWA TAMBIKO LA JUA .
Ilipo
fika saa sita mchana, nikapewa dawa Fulani ya kujipaka, halafu
nikapelekwa kwenye eneo la juani, ambalo chini kuna mchanga.
Hairuhusiwi kuwa katika eneo hilo ukiwa na viatu. Baada ya
kukaa katika eneo hilo kwa kama dakika arobaini hivi , mganga
alianza kufanya uganga wake pale huku akitamka maneno yake ya
kiganga. Baada ya hapo, akanifuata akanikabidhi kibuyu mkononi na
kuniambia nikishike kwa mikono yangu yote miwili kisha nizungumz
nizungumze maneno yafuatayo :
“
EWE JUA! MIMI NA WEWE, TU KITU KIMOJA SASA! WEWE NI MIMI NA
MIMI NI WEWE. HAKUNA MTU YOYOTE YULE AWEZAE KUTUTENGANISHA.
EWE JUA!TANGU UANZE KUWEPO, HAUJAWAHI KUISHIA NJIANI.
VIVYO
HIVYO, MIMI PIA, SITO ISHIA NJIANI. NITAFANYA MAMBO YANGU YOTE,
NITAISHI MIAKA YANGU YOTE KWA KADRI MWENYEZI MUNGU ALIVYO
NIKADIRIA , WALA HAKUNA MTU YOYOTE YULE ATAKAE WEZA KUNIZUIA, KWA
CHOCHOTE KILE NITAKACHO TAKA KUKIFANYA…
KAMA
WEWE JUA UMEWAHI KUISHIA NJIANI, BASI MIMI PIA, NITAISHIA NJIANI.
NA KAMA KUNA MTU ANAWEZA KUKUZUIA WEWE JUA, BASI MIMI PIA
NAWEZA KUZUILIKA. LAKINI KWA KUWA WEWE JUA HAUJAWAHI KUISHIA
NJIANI, MIMI PIA, SINTOISHIA NJIANI. NA KWA KUWA HAKUNA MTU
YOYOTE ANAYE WEZA KUKUZUIA WEWE JUA, BASI MIMI PIA, HAKUNA MTU
YOYOTE ATAKAE WEZA KUNIZUA…
Niliagizwa
kutamka maneno haya mara arobaini. Kila nilipo maliza kutamka,
nilinyweshwa dawa na mganga, kutoka kwenye kibuyu alicho kuwa
nacho…
Baada
ya zoezi hili kukamilika tulirejea kilingeni ili lianze zoezi
la ‘ kumtengeneza’ K, mume wa mtu mwenye pesa.
NAPEWA DAWA ZA KUMTEGA “K”
Tulipo
rudi kilingeni, Mungu wa Kabili akaniambia nimpe majina yangu
kamili pamoja na jina la huyo mwanaume ninae mtaka. Nikafanya
kama alivyo niambia. Akayachukua yale majina, akaandika andika
vitu vyake ambavyo sikuvijua vizuri, baada ya hapo akachukua
kioo chake, akawa anatazama kwenye hicho kioo, kisha akachukua
dawa kutoka kwenye kibuyu, akaweka kwenye chungu ambacho ndani
yake kulikuwa na maji…. Baada ya kama dakika kumi na tano hivi,
akaniangalia halafu akacheka sana.. Akaniambia niweke kiganja
changu kwenye kile chungu nikafanya hivyo..
Basi
akachukua dawa kutoka kwenye vibuyu vitatu, ambazo alizifunga
kwenye vitambaa vitatu tofauti kila kitambaa na dawa yake,
kisha akanipa dawa hizo na kunipa maelekezo yafuatayo : Dawa ya
kwanza, utakunywa na maji ya kawaida, dawa ya pili, utaifunga
kwenye mto unao lalia, halafu dawa ya tatu utaiweka chini ya
kitanda chako.
Ndani
ya siku mbili hizi, kuna kitu utakiona ukiwa umelala usiku.
Kitakujia katika ndoto. Kitu hicho kina uhusiano na mwanaume
unaye mtaka. Uki kiona kitu hicho tu, basi haraka sana nipigie
simu nikuelekeze kitu cha kufanya.. Nikazichukua hizo dawa na
kufanya kama nilivyo elekezwa.
NAMUONA “ K” KWENYE NDOTO.
Siku
ya kwanza sikuona chochote, ila usiku wa siku ya pili, nikiwa
nimelala usiku, niliijiwa na ndoto ya ajabu . Katika ndoto hiyo,
nilimuona K akiwa anatembea kuja mahali kilipo kibanda changu
cha genge.
Alipofika
kwenye kibanda changu alisimama na kuniulizia kama nina hiriki.
Kabla sijamjibu, ndoto ikakatika ghafla… Nilipo stuka na kutazama
saa ilikuwa majira ya saa sita na ushee usiku.
Hapo
hapo nikampigia simu Mungu wa Kabili na kumueleza nilicho
kiona ndotoni… Akaniambia vizuri sana, kisha akaniuliza, je hilo
eneo ambalo umemuona huyo mwanaume akiwa anatembea, unalifahamu.
Nikamjibu ndio nalifahamu. Akaniambia, kesho saa kumi na mbili
alfajiri, nenda kamwagie ile dawa niliyo kwambia uitunze chini
ya kitanda. Baada ya hapo akaninisisitizia, “ Ukiisha fanya nae
mapenzi, uje unione haraka iwezekanavyo, tufanye dawa za
kumfunga..
Nikafanya
kama alivyo nielekeza, alfajiri ya saa kumi na mbili, nikadamkia
katika eneo hilo, kisha nikamwaga ile dawa halafu baada ya
hapo nikarudi zangu nyumbani kujiandaa na kufungua genge langu.
NAINGIA KATIKA UHUSIANO WA KIMAPENZI NA “K” MUME WA MTU.
Saa
mbili asubuhi nilifungua genge langu, nakumbuka siku hiyo
ilikuwa Jumamosi. Mida ya kama saa nne hivi, K alikuja hadi
gengeni kwangu na kununua vitu mbalimbali vya genge, kama vile
karoti, nazi,pilipili manga nakadhalika na kurudi kwake.
Baada
ya kama masaa mawili hivi, K alirejea tena pale gengeni
kwangu, na kuchukua vitu vingine zaidi, halafu akaomba namba
yangu ya simu, aka save namba yangu na mimi nikachukua yake,
kisha akaondoka zake.
Baada
ya kama nusu saa hivi, K akaanza kunitumia meseji za kunisifu.
Alianza kwa kuniambia mimi ni mwanamke mchapakazi, najituma sana ,
nna hasira na maisha , nnafaa kuwa mama kwa sababu hata mume
akifa anakuwa na uhakika watoto wake anawaacha na mwanaume
imara.. Mwisho wa siku akanitongoza, na mimi sikulazia damu.
Kesho yake, mimi na K tukakutana kimwili kwenye hoteli moja
iliyopo maeneo ya Mbezi Beach.
Siku
hiyo K akaniambia niachane na kazi ninayo ifanya, atanitafutia
biashara nzuri ya kufanya, pia nihame pale nilipo kuwa nakaa,
atanipangia nyumba inayo endana na hadhi yake.
NAPEWA DAWA ZA KUMPUMBAZA MUME WA MTU.
Mungu
wa Kabili aliniambia, nikisha fanya mapenzi na huyo mwanaume,
niende kwake ili anipe dawa za kumpumbaza. Nilipofika akaniambia,
vitu vinavyo hitajika katika kutengeneza hiyo dawa ya
kumpumbaza huyo mwanaume, ni NYWELE ZA MWANAUME MWENDAWAZIMU,
NYWELE ZA MWANAUME ASIYE SIKIA ( KIZIWI ) , NYWELE ZA MWANAUME
KIPOFU AU FIMBO ILIYO TUMIWA NA MWANAUME KIPOFU, KAMBA ILIYO
TUMIKA KUMFUNGA KONDOO , pamoja na UCHAFU WA JALALANI.
Vitu
vyote hivyo vilitafutwa vikapatikana, vikachanganywa na dawa
nyingine za kichawi,kisha vikatumika kutengeneza uchawi.
Nikaambiwa nitamuwekea kwenye maji ya kuoga na nyingine
nitamuwekea kwenye chakula .
Halafu
nikapewa na kibuyu, ndani ya kibuyu kile kulikuwa na kipande
cha nyama. Mganga akaniambia hiyo ni nyama ya ndege wa usiku
mwana wa jinni, ambayo baadae nilikuja kujua kuwa ni Bundi wa
Kichawi, ambae ni tofauti na bundi wa kawaida.
Mganga akaniambia utapika nyama, katika nyama utakayo pika
ambayo utamuwekea ndumba, mwanaume wako, utachanganya na nyama
hiyo, pamoja na kucha zako, na nywele zako za siri.
Nilipo rudi nyumbani, nikafanya kama nilivyo elekezwa.
Baada
ya kufanya uchawi huu, K alikuwa kama mwendawazimu kwangu,
hakusikia wala kuambiwa na mtu yoyote Yule. Akawa anafanya kila
ninacho taka akifanye mimi. Akaanza kuwa ananipa mali zake,
magari, viwanja, nyumba, biashara pamoja na miradi yake..
NATEGA UCHAWI WA KUTOA MIMBA YA MKE MWENZANGU.
Mapenzi
yangu na K yalipamba moto, nyumba aliyo nipangishia haikuwa
mbali sana na mahali alipokuwa anaishi yeye na mkewe, wao
walikuwa wanaishi Tabata Mawenzi, mimi akanipangia nyumba nzima
Tabata Kimanga.
K
alihama kwa mke wake, akawa anaishi nyumbani kwangu. Taarifa
za K kuishi na “mchepuko” zilimfikia mke wake, lakini hakuwa
na kitu cha kufanya kwa sababu K alikuwa ndio anamuweka mjini
yeye na familia yake na mwanamke alikuwa mama wa nyumbani tu.
Mara
nyingi K alikuwa ananishauri amfukuze mke wake, ili nikaishi
nae kwenye nyumba yake, ili kuninonyesha kuwa ananipenda sana na
mimi ndio kila kitu kwake.
Ila
kuna kitu kimoja, alinifundisha Mungu wa Kabili, kwamba
unapokuwa mchawi, unatakiwa uwe mnafiki. Usiache kabisa watu
wajue kwamba una jambo Fulani kwa sababu ya uchawi . Hivyo
nikawa najifanya kama namuonea huruma mke wa K lakini moyoni
nilikuwa nataka afukuzwe mimi nikakae, pale.
Kuna
kitu kimoja kilikuwa kinaniumiza moyo. Mke wa K alikuwa na
ujauzito wa kama miezi mitano hivi. Sikutaka mwanamke huyo azae
na K kwa sababu nilijua, angezaa na K mtoto angekuwa
kiunganishi kwao, Mimi nilitaka K akisha achana na mke wake,
basi iwe ndio moja kwa moja na kusiwe na chochote cha
kuwaunganisha. Hivyo nikaanza kupanga njama za kuharibu ujauzito
wa mke wa K kwa kutumia uchawi.
Suala
hili nikalifikisha kwa Mungu Wa Kabili. Mungu wa Kabili
akaniambia nitakupa dawa utaenda kutega kwenye mlango wake. Mti
huo ni wa ajabu sana. Jina lake linafanana na jina la moja
kati ya wilaya zilizopo kusini mwa Tanzania bara.
Baada
ya kupewa dawa hiyo, nikafanya ujanja nikaenda kuitega kwenye
mlango anaoutumia kupita. Alipo ruka mimba ikatoka. Kutoka kwa
mimba ya mke wa K kulinipa sababu ya kurudi kwa mganga kwa
ajili ya kuwatenganisha kabisa K na mke wake. Nilijua, majirani
wangesema K kamuacha mke wake kwa sababu mke ana matatizo ya
uzazi.
NAMTENGANISHA K NA MKE WAKE.
Nikarudi
kwa mganga ili tufanye uchawi wa kumtenganisha K na mke
wake. Mganga alichukua nyoya la ndege ambaye simfahamu jina
lake, pamoja na dawa ambazo sikuzijua pia, akachukua majina ya K
na mke wake, akaenda kuchoma jalalani.
Alipomaliza
hapo, tukaenda kaburini, kwa ajili ya kuuzika rasmi uhusiano wa
K na mke wake. Baada ya kuzika uhusiano wa K na mkewe,
yalifanyika matanga kwa ajili ya kuomboleza “kifo’ cha ndoa ya
K. Mganga alisema, kitu kilicho kufa, kinastahili kupewa maziko
ya heshima. Usipofanya hivyo, roho ya kitu hicho itakusumbueni.
Niliporudi
mjini nikakuta mke wa K kaondoka kwake, kahamia kwa dada
yake. Mimi nikahamia moja kwa moja kwa K nyumba niliyokuwa
nimepangiwa Kimanga nikamuweka mdogo wangu wa kiume.
NAANZA KUFUATILIWA NA NDUGU WA MKE WA ‘K’.
Ndugu
wa mke wa K hawakufurahishwa na kuachana kwa K na mkewe, hivyo
wakafanya kila juhudi kuwapatanisha, lakini msimamo wa K
ulikuwa ni ule ule, kwamba hataki tena kuwa na mke wake na
ameamua kuishi na mwanamke mwingine ambae ni mimi. K alikataa
hata kushiriki kwenye vikao vya usuluhishi. Ndugu wote wa
upande wake na upande wa mke wake wakawa wamemsusia K.
Watu
wawili hawakutaka kukubaliana na matokeo. Nao ni baba wa mke
wa K, pamoja na kaka mkubwa wa mke wa K. Watu hawa waligundua
kilichotokea kati ya K na mke wake sio hali ya kawaida bali ni
nguvu za ushirikina. Hivyo wakaamua kutafuta suluhisho kwa
waganga. Walipo zunguka kwa waganga, hawakufanikiwa, hadi
wakakata tamaa kunidhuru kwa njia ya uchawi.
Mwisho
wa siku wakaamua, kunikodia majambazi, waje wanipige risasi.
Walijua mimi ndio kikwazo kwa mtoto wao kurudiana na mume wake,
hivyo njia pekee ikawa ni kifo tu.
Nilisurika
kuuwawa na majambazi zaidi ya mara saba. Wakati huo Mungu wa
Kabili alikuwa Lubumbashi nchini Kongo kwa shughuli zake. Alipo
rejea nikamfuata kwa ajili ya kuomba ulinzi wake.
Kuna
mnyama mmoja wa mwituni, ana ndimi mbili, yani ulimi wake una
ndimi mbili, Mungu wa Kabili akatafuta ulimi wa mnyama huyo,
mavi ya chatu pamoja na dawa zingine anazo zijua, lengo lake
likiwa ni kuwatenganisha na kuwafarakanisha baba na kaka wa
mke wa K ili wasipate nafasi ya kukaa pamoja na kunifuatilia.
Halafu
baada ya hapo, akaagiza nipeleke mchanga wa kwenye kaburi la
mtu aliyepita duniani bila kuonekana, ili anitengenezee dawa ya
kuwafunga adui zangu wasinione. Pamoja na hivyo, akanipa hirizi
iliyo tengenezwa kwa Mti Mkuu wa Wachawi.
Katika
ulimwengu wa wachawi, mtoto aliye kufa akiwa tumboni kwa mama
ake. Huitwa mtu aliyepita duniani bila kuonekana.
Nilivyo
mpelekea udongo wa kwenye kaburi la mtu aliye pita duniani
bila kuonekana, mganga akauchukua akafanya ulozi wake, halafu
tukaenda wote hadi mtoni, akaenda akatega ndumba zake, pale, kesho
yake tukakuta chura amenasa pale.
Wachawi
wana amini, roho za watoto wanao kufa kabla hawajazaliwa, huwa
zinaenda kuishi mtoni kama Chura. Lakini sio chura wote wapo
hivyo, ni baadhi. Waganga wana utaalamu wao wa kujua chura yupi
anahusika hapo.
Basi
kaka na baba wa mke wa K, walikosana kwa ugomvi mkubwa, kiasi
mtoto akawa anamtukana baba ake mzazi tusi la mama. Na kuhusu
vitisho vya majambazi havikutokea tena
NATUMIA UCHAWI KUOKOA UHUSIANO WA KAKA ANGU.
Kaka
angu ambaye nimempita miaka mitano, alikuwa anaishi kwenye
nyumba ambayo K alinipangia. Nyumba hii ilikuwa maeneo ya
Tabata Kimanga. Kaka angu alikuwa katika uhusiano wa
kimapenzi na mwanamke ambaye alikuwa Baa Medi kwenye bar
inaitwa Mawenzi Garden.
Alimuachisha
kazi ya ubaa medi baada ya mimi kumuwezesha kiuchumi
kutokana na hela na mali nilizo hongwa na K pamoja na kumpa
mradi mmoja wa K ausimamie. Mdogo wangu alimpenda sana mwanamke
huyo .
Ila tatizo moja la mwanamke huyo, alikuwa na tabia ya umalaya. Umalaya ulikuwa kwenye damu yake .
Basi
siku moja mdogo wangu alikuja kwangu kunishitakia kuhusu tabia
ya wifi yangu. Mdogo wangu alikuwa anampenda sana mwanamke
huyo, na alikuwa hawezi kumuacha kwa sababu yoyote ile, ila
alikuwa anamuumiza sana kwa sababu ya tabia yake ya umalaya.
“
Ninampa kila kitu huyu mwanamke, ninampa hela, nimemfungulia
biashara, nimempa gari, nawasomesha wazazi wake na kusaidia
familia yake,. Lakini haridhiki tu, mwisho wa siku anatumia hela
ninazo mpa kuhonga wanaume wengine.. ( HELA , GARI NA VITU VYOT
AMBAVYO MDOGO WANGU ALIKUWA AKIMPA WIFI YANGU, VILIKUWA MALI
YA K ALIZO CHUMA KWA JASHO LAKE NA MKE WAKE)
Nilimuonea
huruma sana mdogo wangu, na nikaamini sio akili yake ila
atakuwa amerogwa na mwanamke Yule. ( UNAJUA UKIWA MSHIRIKINA,
KILA KITU UNAKUWA UNAAMINI KIMESABABISHWA NA USHIRIKINA )
Nikamwambia
mdogo wangu usijali, kesho nitakwenda Bagamoyo kwa mtaalamu
wangu, nitamuelezea tatizo lako, halafu nitamsikia atakacho
niambia, nitakujulisha, ila usijali kama mwanamke huyo
amekufanyia mambo ya Kiswahili, itajulikana tu na utakuwa huru.
Nilipo
fika kwa Mungu wa Kabili, nikamueleza kila kitu, akaniomba
majina ya mdogo wangu pamoja na jina la huyo wifi yangu,
akatazama kwenye radar zake, halafu akacheka sana.
Mungu
wa Kabili akaniambia, hakuna haja ya kumfunga mwanamke huyu.
Huyu mwanamke ana sumbuliwa na damu ya umalaya. Umalaya upo
kwenye damu yake. Hata tukimfunga kwa mdogo wako, tutakuwa
tunajisumbua tu, atampenda sana mdogo wako, lakini atatoka nje tu
kwa wanaume wengine. Hapa cha msingi, afanyiwe dawa ya kumfanya
aache umalaya.
Mungu
wa Kabili akachukua dawa moja inaitwa GEGEZI. Hii Gegezi ina
ukubwa kama tunda linaitwa DADANSI na ina mibamiba.
Halafu
akachukua dawa nyingine ambayo ni chakula cha ndege mmoja wa
porini. Ndege huyo simkumbuki jina lake, ila ni mweusi, ana mdomo
mrefu, ndege huyu akilia, vinyonga wote waliopo katika eneo
hilo wanakimbia, huwa anakula vinyonga pia.,
Sasa
ndege huyu huwa anakula majani ya mti Fulani wa porini ambao
nimeusahau jina lake, hayo majani ndio ambayo Mungu wa Kabili
aliya chukua.
Kitu
kingine akachukua majani Fulani hivi, hayo majani ndio majani
pekee yanayo liwa na mnyama wa porini ambae chakula chake
kikuu ni nyama.
Pamoja
na dawa hizo akachanganya na dawa zake nyingine ambazo
sikuweza kujua ni dawa gani, halafu akaagizwa itafutwe minyoo
ipatayo saba. Vito vyote hivyo vikaunguzwa pamoja kwenye chungu,
hadi vikawa unga unga halafu vikachanganywa na mafuta ambayo
sikujua ni mafuta ya kitu gani.
Mungu
wa Kabili akanipa dawa hiyo akaniambia mpelekee kaka ako.
Mwambie akiwa anafanya mapenzi na huyo mwanamke wake, afanye
ujanja wake, achovye kidole chake kwenye hiyo dawa halafu
akichomeke kwenye uke wa mwanamke huyo.
Tangu
siku hiyo, mwanamke huyo hatokuwa Malaya tena . Nikafanya kama
alivyo nielekeza na tangu mdogo wangu afanye hivyo, sikuwahi
kumsikia tena akinipa kesi za wifi yangu, zaidi ya kumsifia
mpenzi wake ametulia. Mwisho wa siku walifunga ndoa na kuzaa
watoto.
NAMTEKA KICHAWI KIJANA WA KIARABU.
Nilimroga
K kwa sababu ya pesa zake. Nikiwa kama mwanamke kamili,
nilihitaji kuwa na mwanaume ninaye mpenda kutoka moyoni mwangu.
Nataka nitoe funzo moja kwa wanaume, mnajua kila mwanamke alie
olewa ambae hajaokoka huwa ana wanaume wawili. Mwanaume wa
kwanza ni mwanaume ambae yupo nae katika ndoa, na mwanaume wa
pili ni mwanaume ambae alitamani awe nae katika ndoa. Hivyo
ndivyo ilivyo kuwa kwangu.
Sasa
basi, kuna kijana mmoja wa kiarabu ambae nilikuwa namzidi umri
kwa miaka minane. Kijana huyu aliishi mtaa wa pili kutoka
nyumba niliyo kuwa nikiishi na K.
Nilitokea
kumpenda sana kijana huyo lakini sikuwa na namna ya kumuanza,
mnajua mwanamke kumtongoza mwanaume sio kazi rahisi. Nikaona
isiwe tabu nikaamua kwenda kwa Mungu wa Kabili, ili anipe
ndumba za kumnasa kijana huyo ambae kwa jina aliitwa Feisal.
Nilipo
fika kwa Mungu wa Kabili akaniambia “ Inaonekana wewe ni mtundu
mtundu sana,. Halafu naona una mambo mengi. Sasa
nitakutengenezea uchawi, ambao utakuwa unautumia mwenyewe kumnasa
mwanaume yoyote unae mtaka. “. Mungu wa Kabili akaniambia, njia
hiyo itakuwa bora kuliko mimi kuwa naenda kumuona kila mara
kwa jambo lile lile.
Mungu
wa Kabili akaniambia, nitafute kopo linalo tumika chooni,
nitafute nguo za marehemu. Hapa simaanishi nguo za maiti, la
hasha nina maanisha nguo za marehemu.
Mfano
wake ni kwenu kuna mtu amefariki, nguo zake zimegawiwa kwa
ndugu, jamaa na marafiki, sasa nguo hizo ndio anazo zitaka.
Mungu
wa Kabili, akaniambia niwe na uhakika kwamba nguo nilizo pewa
ni nguo za marehemu kweli, hilo la kwanza, lakini pili niwe
na uhakika kwamba marehemu huyo alikufa kifo cha Mungu na
sio kachukuliwa msukule.
Nikamuuliza
nitajuaje kuhusu mambo hayo, akaniambia ni rahisi sana. Wewe
ukizipata nguo za marehemu, au mtu atakae kuuzia nguo za
marehemu, basi akuonyeshe mahali lilipo kaburi la marehemu,
halafu utakuja kwangu nikuelekeze cha kufanya.
(
KATIKA ULIMWENGU WA WACHAWI, NGUO ZA MAREHEMU NI BIASHARA
KUBWA SANA, KUNA WATU WANAISHI KWA KUFANYA BIASHARA YA KUUZA
NGUO ZA MAREHEMU MBALIMBALI..MIMI MWENYEWE NILIUZIWA NGUO ZA
MAREHEMU KWA BEI MBAYA ).
Baada
ya kufanikiwa kupata nguo za marehemu, pamoja na kuonyeshwa
mahali lilipo kaburi la huyo marehemu, nilirejea kwa Mungu wa
Kabili.
Mungu
wa Kabili alizichukua zile nguo, akakata kipande kidogo kwenye
shati moja, akapaka mafuta ambayo sikujua ni mafuta ya nini,
akazifunga kwenye kitambaa chekundu, akaweza kwenye kibuyu, ndani
ya kibuyu hicho akaweka yai la kuku mweusi, sindano saba pamoja
na mafuta mengine ambayo sikujua ni mafuta ya nini ila wao
wachawi na waganga wanayaita mafuta ya usiku, kisha akakifunga
kile kibuyu, halafu akanikabidhi, akaniambia, ikifika usiku wa saa
moja , nenda hadi kwenye hilo kaburi, kisha ukiweke kibuyu
hicho juu ya hilo kaburi kwa kukilaza., halafu asubuhi pita
katika kaburi hilo uangalie kwa makini kibuyu hicho, ukikikuta
bado kimelala kama ulivyo kiacha basi ujue huyo marehemu kweli
amekufa kifo cha Mungu, lakini ukikuta kimesimama, basi marehemu
huyo bado yupo hapa hapa duniani, amechukuliwa msukule.
Nikafanya
kama alivyo niagiza, na kweli kesho yake nikakuta kibuyu
kimelala kama nilivyo kiweka. Mungu wa Kabili akaniambia nguo
hizo zinafaa kwa ajili ya kutengeneza dawa hiyo.
Basi
akachukua hizo nguo, akaziunguza kwenye chungu cheusi pamoja na
dawa nyingine kama aina kumi na mbili, halafu akazihifadhi
kwenye kibuyu na kunikabidhi, pamoja dawa zingine kwenye vifuko
vitatu.
Akaniambia,
ukimtaka mwanaume yoyote Yule, utamuita kwa kutumia dawa hii…
Mwanaume utakae muita sauti yako ataisikia na kuitii mara moja
kama ambavyo marehemu huyo alivyoitwa na Mungu na kuitii
sauti yake.
Mungu
wa Kabili akaniambia huo ni uchawi mkubwa sana katika
mapenzi, hakuna mwanaume nitakae muita na akakataa kuitika.
Uchawi huu hautumiki katika mapenzi tu, hata kama mambo mengine,
ilimradi unacho taka wewe ni kumuita mtu.
Kitu
kingine akaniambia, ukimuita mwanaume kwa kutumia uchawi huu
zaidi ya mara saba, halafu akakataa kuitika, basi jua kwamba
mwanaume huyo kinga yake ni kubwa sana.
Sasa
basi ukisha ligundua hilo, unatakiwa kutuma nyoka wa kichawi
kuua kinga ya mwanaume huyo. Ukisha ua hiyo kinga, muite tena
mwanaume huyo na atakuja haraka sana.
Nyoka
huyu sio nyoka wa kawaida kama nyoka wengine. Ni nyoka wa
kichawi. Ni jinni. Mungu wa Kabili akanikalisha kwenye kigoda na
kuniambia, “ Nitamtengeneza nyoka huyu, halafu nitakukabidhi,
umtunze vizuri kwa kufuata masharti yake…”
Katika
kumtengeneza nyoka wa kichawi, Mungu wa Kabili akachukua kitovu
cha mtoto. ( KUWENI MAKINI SANA NA MAHALI MNAPOVITUPA VITOVU VYA
WATOTO WENU.. KATIKA ULIMWENGU WA WACHAWI VITUVO VYA WATOTO NI
BIASHARA KUBWA SANA… KITOVU CHA MTOTO KINAPOENDA KUTUPWA, AMA
KUFUKIWA, KATIKA WATU WANAO PEWA JUKUMU LA KUVITUPA, HUWA KUNA
MMOJA WAPO ANAWEZA KUWA SIO MUAMINIFU, HUENDA KUFUKUA MAHALI
KILIPOFUKIWA NA KWENDA KUKIUZA KWA WACHAWI NA WAGANGA )
Alipochukua
hicho kitovu, akakifunga kwenye mti wa mnyonyo, halafu
akanyunyizia dawa kutoka kwenye vichupa kama saba. Baada ya
hapo akachukua uzi mwekundu, akafunga vifundo saba kwenye kamba
hiyo, halafu akatupa kwenda chini, ilipotua tu, ikageuka kuwa
nyoka. Akamshika huyo nyoka, akamuhifadhi kwenye kibuyu cheusi,
chenye shanga juu, akafunga na kitambaa cheusi na kunikabidhi..
Akanielekeza jinsi ya kumtuma nyoka huyo kufanya kazi
mbalimbali pamoja na masharti yake.
Kuhusu
lile kopo la chooni, Mungu wa Kabili akaniambia amelitumia
kutengeneza dawa ya kujua siri za watu. Dawa hiyo itanisaidia
kujua kama mwanaume niliye nae ana hela au hana hela, ana mke
au hana mke. Ana watoto au hana watoto.
Kingine
akanikabidhi ua ambalo natakiwa kulipanda nyumbani. Kupitia ua
hilo nitakuwa ninajua kama mwanaume ambae nipo nae amepata hela
au la.
Kitu
cha mwisho, akaniambia, kwa sababu nnaonekana nnapenda sana
wanaume, inabidi anipe dawa ya kuwatengeneza wanaume nitakao kuwa
nao na kuwafanya kutokuwa na uwezo wa kufanya mapenzi na
wanawake wengine isipokuwa mimi tu. Hii itasaidia kuniepusha
na magonjwa kama vile ukimwi nakadhalika.
Mungu
wa Kabili akanipa mti mmoja mrefu, akaniambia katika mti huo,
utatumia zaafarani nyekundu au ya njano, kuandika majina ya
wanaume wote ambao upo nao kimapenzi pamoja na jina lako,
ukisfanya hivyo, nenda kautegeshee barabarani, ukishagongwa na
gari tu, basi wanaume hao watakuwa wakikutana na wanawake
wengine, uume wao unakuwa haufanyi kazi.
Nilivyo
rudi nyumbani nikafanya kama nilivyo elekezwa na kweli Yule
kijana alikuja mara moja tangu nilipo muita. Nilifurahi sana
kumpata Feisal. Pamoja na kwamba nilikuwa nimemuita kichawi ila
nilikuwa namuheshimu sana kwa sababu nilikuwa nampenda toka
moyoni mwangu.
Baada
ya kama wiki mbili tangu nianzee uhusiano wangu na Feisal,
nikagundua Feisal ana tatizo la ukosefu wa nguvu za kiume.
Uwezo wake kitandani ulikuwa mdogo sana.
Kama
kawaida yangu nikaenda kumuona Mungu wa Kabili. Mungu wa
Kabili akanipa dawa moja inaitwa KISHINDO. Akaniambia utakuwa
unachemsha unampa anakunywa glasi moja asubuhi na nyingine
anakunywa jioni, kwa siku kumi mfululizo. Nikafanya kama alivyo
nielekeza. Baada ya kumpa Feisal dawa hiyo, nilijilaumu kwanini
nilifanya hivyo. Uwezo wake kitandani ulikuwa wa ajabu, alikuwa
anashiriki tendo kwa muda mrefu sana na alikuwa akirudia mara
nyingi bila kuchoka…
NAMFANYIA VITUKO K
Katika
muda wote huo, nilikuwa bado ninaishi na K kwenye nyumba yake
ya Tabata Mawenzi. K alikuwa kama Ndondocha kwangu. Kwanza
nilikuwa simpi unyumba na nilikuwa nafanya kila kitu ninacho
taka kukifanya tena mbele yake.
Feisal
alikuwa anakuja nalala nae chumbani, K analala pepe yake
kwenye chumba kingine. Alikuwa anafanya kazi zote kama vile
kufua, kufanya usafi na kila aina ya kazi ambayo houseboy
anatakiwa kuifanya.
Na
katika kipindi hiki K alikuwa ameshafukuzwa kazi kutokana na
uzembe kazini. Mimi mwenyewe nilimpiga marufuku kwenda kazini
kwa mwezi mmoja, nilimwambia achague kitu kimoja kati ya kwenda
kazini au kufanya kazi zangu.
Sasa
basi nikawa namfanyia K vituko, lengo langu nikitaka aondoke
mwenyewe aniachie nyumba na mali zake. Hakuwa na faida yoyote
tena kwangu. Kazi ameshafukuzwa , mali zake zote pamoja na
biashara zake ninazimiliki mimi.
Basi
kila nilipokuwa nikifanya mapenzi na Feisal nikawa napiga
kelele ili kumuudhi K. Na hivi Feisal alikuwa anatumia muda
mrefu basi na kelele zangu zikawa za muda mrefu. Lakini wapi, K
wala hata hakuonyesha dalili ya kwamba anaweza kuondoka ,
undondocha ulikuwa umetamalaki kwenye kichwa chake.
Kwa
kutumia ndumba hizo nilizo pewa na Mungu Wa Kabili, niliwateka
kichawi wanaume wengi na kuvunja ndoa nyingi sana.
K ANAAMUA KURUDI KIJIJINI
Nilipoona
K hana dalili ya kuondoka pamoja na kumfanyia vituko lukuki,
nikaona niende kwa Mungu wa Kabili ili kama kuna uwezekano wa
kumfukuza K kichawi.
Nilipofika
kwa Mungu wa Kabili, akafanya dawa zake, halafu ikatengenezwa
ngalawa ndogo, nikaambiwa nipeleke nguo yoyote ya K . Nguo ya K
ikafanyiwa uchawi halafu ikafungwa kwenye hiyo ngalawa, tukaenda
baharini kutegea wakati bahari imesafiri tukaenda kuiweka ngalawa
, maji yalipokuja yakaondoka na hiyo ngalawa, kesho yake tu, K
mwenyewe akasema anataka kwenda kusalimia kijijini kwao
amepakumbuka. Nilifurahi sana niliposikia hivyo, nikamfungia nguo
zake, nikampa na nauli pamoja na hela ya kula njiani..
K
alivyo rudi kwao, baadhi ya ndugu zake hawakuridhishwa na hali
ya K pamoja na maelezo yake. Mtu aliyekuwa tegemeo la ukoo
mzima, ghafla anarudi kijijini akiwa hana kitu na maelezo yake
yanatatanisha. Wakaamua kufunga safari hadi mjini ili
kufuatilia mali za ndugu yao. Nilipo pata taarifa zao, nikaenda
kuwashitaki kwa Mungu wa kabili, wote walipeperuka na sikusikia
chochote kuhusu watu hao.
NAINGILIA NDOA YA WALOKOLE.
Nilitokea
kumtamani mwanaume mmoja mlokole alieishi mtaa wa pili
kutokea nilipokuwa naishi. Huyu nilimpenda kama nilivyo mpenda
Feisal. Alikuwa mkaka mzuri anae jipenda sana. Kwa jina aliitwa
Erasto. Kikwazo kikubwa kwa Erasto ilikuwa, kwanza alikuwa
ameokoka na pili alikuwa na mke ambaye alikuwa ameokoka pia. Mke
wa Erasto alikuwa na ujauzito mkubwa tu wa kama miezi mitano
au sita .
Nasema
kuokoka ilikuwa kikwazo kwa sababu Mungu wa Kabili Alisha
nishauri niwe makini sana na walokole kwa sababu wana nguvu
za ajabu. Ila akaniambia kuna walokole wa waina mbili., mlokole
wa ukweli na mlokole feki. ..
Hivyo
basi kama umemempenda mwanaume wa kilokole, unatakiwa kwanza
umpime kichawi kujua kama ni mlokole wa ukweli ama mlokole
feki.
Akaniambia
uchawi unao tumika kupima nguvu ya mlokole, sio uchawi wa
kitoto, hauwezi kufanywa na mtu yoyote, akaniambia kama
itatokea nimempenda mwanaume wa kilokole, basi niende kwake
halafu yeye atampima kama mlokole huyo ni orijino au feki..
Kama ni orijino una achana nae kwanza unatafuta njia nyingine
ya kumpata, lakini kama ni feki,unamvuta kama watu wengine.
Akaniambia,
ukimpenda mwanaume wa kilokole orijino ni bora utumie njia za
kawaida kumteka, kuliko njia za kichawi, kwa sababu kwa njia
za kawaida, ataishia kukukemea tu,. Lakini kwa njia ya uchawi,
utapigwa shot. Hakuniambia ni shoti gani.
TUNATUMIA UCHAWI KUPIMA ULOKOLE WA ERASTO.
Ili
kujua kama mlokole ni orijino au feki, wachawi hutumia nzi.
Hivyo basi Mungu wa Kabili alianza kufanya uchawi ili kupima
kama Erasto ana nguvu za Mungu au hana nguvu za Mungu.
Siku
hiyo Mungu wa Kabili akachukua bakora ya kichawi ambayo
imetengenezwa kwa mti wa Mkomoro, Mganga akaniambia mti huo wa
mkomoro ni mti wenye nguvu nyingi sana za kichawi na wachawi
huutumia kwa mambo mengi ikiwa ni pamoja na kufufua wafu.
Mungu
wa Kabili akaanza kwa kuwaita inzi na kisha kuwatuma waende
kwa Erasto ili kujua kama ana nguvu za Mungu au la. Lilikuja
kundi la nzi wengi, na walipo tua tu kwenye fimbo yake wote
wakapasuka pale pale.
Mungu
wa Kabili akaniambia kwa kunisisitiza, achana kwanza na huyu
Erasto, kesho ninasafiri kwenda Mkuranga , nitakuwa huko kwa
siku saba tunaenda kupika uganga . Nitakapo rudi tutaangalia njia
nyingine ya kumteka Erasto.
Waganga
na wachawi huwa wanakuwaga na MWAKA WA UCHAWI ama MWAKA WA
UGANGA, kama ambavyo kuna MWAKA WA FEDHA, MWAKA WA MASOMO
nakadhalika.
Unapofika
mwaka wa uganga, waganga hukutana mzimuni na kupika uchawi,
ambao huuzwa kwa waganga mbalimbali. Jambo hilo hufanyika
kila mwaka.
Mungu
wa Kabili alikuwa anaelekea Mkuranga kwa ajili ya kusimamia
zoezi la upikaji wa uchawi unaoitwa MANGUBE. Kwa hiyo Mungu
wa Kabili akaniambia nisubiri kwanza mpaka wiki mbili zipite ndio
tuje tukae tupange cha kufanya juu ya Erasto, kwa sababu
baada ya kutoka Mkuranga alikuwa anaelekea Liwale Lindi.
Sikuwa na jinsi zaidi ya kukubaliana na maagizo ya Mungu wa Kabili.
NAMTUMIA ERASTO NYOKA WA KICHAWI.
Baada
ya siku tatu uvumilivu ukanishinda, nikaamua liwalo na liwe,
kama kuna baya litanitokea, Mungu wa Kabili atanisaidia.
Usiku
wa saa sita siku hiyo, nikamchomea Erasto, dawa ya kumvuta
kwangu kichawi. Kwa kawaida nikishachoma dawa, usiku huwa naota
nafanya mapenzi na mwanaume nilie mchomea dawa na kesho yake,
kabla ya saa sita mwanaume huyo huwa ananitafuta, lakini kwa
Erasto ikawa tofauti. Sikuona chochote. Nikachoma kwa siku saba
mfululizo hakuna chochote.
Nikakumbuka
Mungu wa Kabili aliniambiaga kwamba, kama nikichoma dawa ya
kumuita mtu na mtu huyo asije, basi nijue kuwa mtu huyo ana
kinga kubwa, kwa hiyo natakiwa nimtumie nyoka wa kichawi, nyoka
huyo ataenda kuvunja kinga ya mtu huyo.
Siku
hiyo usiku wa saa sita, nikaenda kuchukua kile kibuyu ambacho
kilitumika kumuhifadhi Yule nyoka, nikamtuma nyoka huyo aende
kuigonga na kuivunja kinga ya Erasto. Nilipomaliza kunena maneno
yangu nikafungua kile kibuyu ili nyoka atoke, nyoka alipotoka
akanigonga kwenye mguu na kutokomea.
Nilipiga
kelele za ajabu, house girl wangu akaenda kuwaamsha majirani na
kupiga simu ya kaka angu, nikapelekwa hospitali, hospitali
nikapimwa lakini hakikuonekana kitu, wala haikuonekana kama nina
sumu yoyote mwilini, lakini nilikuwa nasikia maumivu makali sana
yaliyokuwa yanakuja na kuondoka, nikapewa dawa za kuzuia maumivu
lakini wapi. Ilipofika asubuhi maumivu yakawa yameisha lakini
nikawa nimepooza upande mmoja.
Nikamwambia
kaka angu apige simu ya Mungu wa Kabili, lakini Mungu wa
Kabili alipopigiwa na kuelezewa kilicho tokea, akawa mkali sana,
kwanza akasema alinionya nisifanye chochote halafu pili akasema
hawezi kunisaidia kwa namna yoyote ile.
Sikuwa
na jinsi zaidi ya kumueleza kaka angu ukweli. Kilicho fuatia
tukaanza kuzunguka kwa waganga wa kienyeji kwa ajili ya tiba
yangu lakini wapi. Baada ya wiki mbili nilipelekwa kwa Mungu wa
Kabili Bagamoyo angalu aione hali yangu ilivyo labda anaweza
kunionea huruma lakini, akakataa kata kata…. Msimamo wake ulikuwa
ni ule ule, nimefanya jambo ambalo alinikataza kulifanya na
pia hana uwezo wa kunisaidia. Zaidi aliniambia hatima yangu ni
kifo.
Tulizunguka kwa waganga wa kila aina na kila sehemu lakini wapi hali yangu ikazidi kuwa mbaya.
Siku
moja ndugu yangu mmoja wa upande wa mama angu, alikuja
kuniona baada ya kusikia nimepooza. Baada ya kumsimulia kuhusu
kisa changu alisikitika sana. Nikapelekwa kwenye kanisa moja la
kiroho na kuombewa. Siku tatu tangu nianze kuombewa nilitapika
vitu vingi sana vya ajabu ajabu, kama vile kucha, nywele, damu
nakadhalika, na taratibu hali yangu ikaanza kutengemaa na
hatimaye nikapona kabisa.
Namshukuru
Mungu sasa hivi nimeokoka, nimempokea Yesu kama Bwana na
Mwokozi wa maisha yangu. Mali za K nimezirudisha na sasa
ninaishi maisha yangu halali kwenye chumba cha kupanga maeneo ya
Mbezi Ya Kimara.
Ninaumia
sana moyoni kuona, nimeseababisha mateso kwa wanawake wenzangu,
nimevunja ndoa za watu. Nimeamua kumtumikia Mungu katika
maisha yangu yote. Ninawaomba msamaha wale wote nilio waharibia
maisha.
CHA
MWISHO NA KIKUBWA.. NAWATAHADHARISHA WANAWAKE WENZANGU KUHUSU
WAGANGA WA KIENYEJI, HUSUSANI HUYU ANAEITWA MUNGU WA KABILI. NI
MTU HATARI SANA NA MCHAWI MKUBWA. NAOMBA MSIENDE KUFUATA
MSAADA WAKE JAMANI KWA SABABU NI MCHAWI.. NAMBA ZAKE ZA SIMU
NI 0744 000 473. MSIPIGE NAMBA HIYO JAMANI, YATAWAKUTA KAMA
YALIYO NIKUTA MIMI. NIMEONA NIWEKE NAMBA ZAKE HADHARANI ILI
MZIJUE NA KUJIEPUSHA NAZO, KWA SABABU NAONA ANATANGAZWA NA
VYOMBO MBALIMBALI VYA HABARI. NAOMBA KILA ATAKAE PATA UJUMB HUU,
AMJULISHE NA MWENZAKE
YESU AWAONGOZE NA AWALINDE.
0 Maoni:
Post a Comment