Mbunge
wa Temeke Mhe. Abdalah Mtolea jana alipandishwa kizimbani katika
mahakama ya wilaya ya Temeke akikabiliwa na mashataka mawili ikiwemo la
kuendesha gari bila ya bima kinyume na sheria za nchi.
Mbunge
huyo kwa tiketi ya chama cha wanachi CUF, alisomewa mashtaka yake mbele
ya hakimu mkazi Mhe. Eliarusia Nassatri mbale ya mwendesha mashtaka wa
serikali Joseph Maugo ambaye aliiambia mahakama hiyo kuwa katika kosa la
kwanza Mbunge huyo anadaiwa kuendesha gari ambalo halina bima
Maelezo
ya kosa hilo yanadai kuwa, Julai 19 mwaka huu katika barabara ya Kilwa
eneo la Bendera tatu, mshtakiwa alikuwa akiendesha gari lenye namba za
usajili T 672 BNV Toyota Mark 2 likiwa halina bima.
Katika
kosa la pili, mshatakiwa Mtolea anadaiwa kulitenda muda na eneo la
kwanza alipotenda kosa la kwanza kwakushindwa kutekeleza agizo la ofisa
Polisi mwenye namba F 818 Kopla Robati la kutakiwa kupeleka gari hilo
katika kituo cha Polisi Kilwa Road lakini mshtakiwa alikaidi agizo hilo
na kuelekea maeneo ya katikati ya jiji.
Baada
ya kusomewa makosa hayo, Mtolea alikiri makosa yote ambapo alisomewa
maelezo ya awali (PH) kisha kuhukumiwa kulipa faini ya Pound 100 na Tsh.
30,000.
Katika
hukumu yake, Hakimu Nassary alisema, kosa la kwanza mshtakiwa anatakiwa
kulipa Pound 100 sawa na Tsh. 291,700 au kifungo cha miezi 6 jela
wakati kosa la pili ni kulipa faini ya Tsh. 30,000 au kifungo cha miaka 2
jela ambapo baada ya kutolewa hukumu hiyo, Wakili wa utetezi Hashim
Mziray aliieleza kuwa mteja wake atalipa faini hiyo.
0 Maoni:
Post a Comment