Rais
wa Jamuhuri wa Muungano Wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli
amempongeza aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini, David Kafulila
kutokana na namna alivyojitoa katika kutetea maslahi ya Watanzania
kwenye sakata la Escrow(IPTL) na kuonesha uzalendo mkubwa ambao hawezi
kusahaulika katika historia ya Tanzania.
Rais
Magufuli ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wakazi wa Kata ya
Nguruka katika hafla ya uzinduzi wa mradi mkubwa wa maji uliopo Tarafa
ya Nguruka katika Wilayani Uvinza ambapo alisema kuwa akiondoka hapo
bila kumpongeza Kafulila atakuwa amefanya dhambi ya unafiki
itakayompeleka motoni.
Akizungumza,
Rais alisema anatambua kwamba Kafulila yupo chama kingine, lakini
kwenye suala la IPTL, aliweka maslahi ya Taifa mbele na kusimamia ukweli
hivyo anampongeza na pongezi hizo ni za dhati kwani zinatoka moyo. Rais
alieleza umma uliokuwa umejitokeza mahali hapo kuwa, wizi uliokuwa
unafanywa na IPTL ni mkubwa hivyo Kafulila alisimama kutetea umma wa
watannzani.
Lakini
pia Rais alieleza vikazwo ambavyo Kafuli alikutana navyo wakati
akipambana kuhusu wizi huo uliokuwa ukiratibiwa na baadhi ya watumishi
wa serikali kwa manufaa yao wenyewe.
“Wakamtisha
wengine kumpeleka mahakamani, wakamtukana wee, wengine wakamuita
tumbili, sasa tumbili amefanya makubwa kwa ajili ya Watanzania. Wao ndio
matumbili, huyu (Kafulila) alifanya kazi ya Mungu ya kuwatumikia
Watanzana,” alisema Rais Magufuli huku wakazi wa eneo hilo wakilipuka
kwa furaha.
Akiendelea
kumwaga sifa hizo za dhati, Rais Magufuli alisema kwenye hili suala la
wizi wa IPTL, atampongeza Kafulila kwa maisha yake yote.
Akizungumzia
suala la uzalendo, Rais amesema nchi ilikosa uzalendo na kwamba kila
aliyekuwa akichaguliwa alikazana kukusanya mali zake yeye mwenyewe bila
kujua kuwa atakufa na atazikwa kwenye shimo moja, hivyo akawasihi
watanzania wajenge uzalendo.
Alisema
maendeleo hayana chama na kwamba, kiongozi mzuri ni yule anayewatumikia
watu wake bila kujali chama, kwani mradi huo wa maji anaoufungua
utanufaisha watu wote hata wasio na chama. Alieleza kwamba, ushabikia
wa vyama ndio unaochelewesha maendeleo ya watanzania.
Rais
Magufuli amemaliza ziara yake ya kikazi ya siku tatu Mkoani Kigoma kwa
kuweka jiwe la msingi katika mradi wa Maji mkubwa katika kata ya Nguruka
uliogharimu zaidi ya shilingi bilioni 2 ambao unatarajiwa kukamilika
Disemba 30 mwaka huu ambao utafuta kero ya maji kwa wananchi wa kata ya
Nguruka.
0 Maoni:
Post a Comment