MGOMBEA
nafasi ya Uenyekiti katika Klabu ya soka ya Lipuli Fc 'Wanapaluhengo,
Abinery Mrema (kushoto) amewaahidi wanachama na wapenzi wa soka mkoani
hapa atahakikisha timu hiyo inamiliki uwanja wa mazoezi endapo
atachaguliwa.
Akizungumza na dmgidange.blogspot.com jana , Mrema alisema kuwa timu ya Lipuli ambayo kwa sasa iko ligi
kuu Tanzania Bara haina budi kuondokana na viwanja vya kuazima kwa ajili
ya kufanyia mazoezi hivyo atahakikisha timu hiyo inapata uwanja wake.
Alisema
kuwa licha ya kuwa uwanja wa mazoezi atahakikisha inawekeza katika
vitega uchumi ambavyo ni kuwa na kiwanja kwa ajili ya uwekezaji, kuwa na
chuo cha mafunzo kwa watoto, na kuhakikisha timu hiyo inapata usafiri
wa uhakika.
Aliongeza
kuwa atahakikisha wanafungua matawi ya timu ya Lipuli nchi nzima na nje
ya nchi ambapo watachangia kwa kiasi kikubwa kukuza uchumi wa timu ya
Lipuli .
"Nitahakikisha
timu ya Lipuli inakuwa na matawi mengi ndani na nje ya nchi na
nitahakikisha nawashawishi wadau wakubwa wa ndani na nje kuweza
kuisaidia timu yetu ili iweze kufanya vizuri katika ligi" alisema
Mrema
alisema kuwa endapo wanachama watampatia ridhaa ya kuongoza timu ya
Lipuli Fc atahakikisha wanafanya mikutano ya mara kwa mara na wadau
kuwaelezea maendeleo ya timu na changamoto zake kwa lengo la kupata
ufumbuzi.
Aliongeza
kuwa atahakikisha Lipuli inafaidika na nembo ya timu katika kwa kuingia
mikataba yenye maslahi kwa timu hasa katika uuzwaji wa vifaa vya timu
kama Jezi.
Uchaguzi
wa nafasi mbalimbali za uongozi wa timu ya Lipuli unatarajiwa kufanyika
Julai 23 mwaka kwa nafasi za Uenyekiti, Makamu na ujumbe wa kamati.
0 Maoni:
Post a Comment