Manchester United yaichapa Real Madrid kwa penalti

Timu hizi zitakutana katika mchezo wa super cup Agosti 8
Manchester United wameifunga Real Madrid kwa mikwaju ya penalti baada ya kumaliza dakika 90 kwa sare ya goli 1-1.

Anthony Martial alitumia juhudi binafsi na kumtengenezea pande Jesse Lingard na kuandika goli la kwanza.

Casemiro aliisawazishia Madrid kwa njia ya penalti baada ya mlinzi mpya wa United Victor Lindelof kumuangusha Theo Hernandez katika eneo la hatari.

Penalti saba kati ya kumi hazikuingia nyavuni.
Casemiro alikosa mkwaju wa penalti kwa kugonga mwamba wa juuCasemiro alikosa mkwaju wa penalti kwa kugonga mwamba wa juu 

Haukuwa usiku mzuri kwa Lindelof ambaye aliendeleza makosa yake na kukosa mkwaju wa penalti.

United wameshinda michezo yote minne katika ziara nchini Marekani na watakutana na Barcelona katika fainali siku ya Jumatano.
 
Share on Google Plus
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment