Akielezea
tukio hilo leo (Alhamisi Julai 6) , Mkuu wa Operesheni Maalumu za
Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Liberatus Sabas amesema
tukio hilo lilitokea jana saa nne usiku katika msitu wa Ngomboroni
Kata ya Ikwiriri, Wilaya ya Ikwiriri.
Wahalifu hao
waliuawa na askari wa operesheni maalumu wakiwa katika doria za
ufuatiliaji wahalifu sugu wanaojihusisha na mauaji yanayoendelea katika
kanda hiyo ya kipolisi.
Alisema askari wakiwa na
mtuhumiwa mmoja muhimu anayeshiriki katika mauaji hayo ambaye
alikamatwa, alikubali kwenda kuwaonyesha polisi mahali ambapo ni
maficho ya wenzake.
“Baada ya kufika eneo la msitu wa
Ngomboroni kikundi cha watu wanaokadiriwa kufikia watano walikurupuka
kutoka kwenye kichaka na kuanza kukimbia ndipo polisi kwa tahadhari
kubwa walianzisha mashambulizi na kufanikiwa kumjeruhi mhalifu mmoja kwa
risasi, katika mashambulizi hayo mtuhumiwa aliyekuwa mkononi mwa
polisi naye alijaribu kutoroka na hivyo kupelekea kumjeruhi kwa risasi
hivyo idadi yao kufikia wawili,” amesema.
Ameongeza;
“majeruhi hao wawili walifariki dunia njiani wakati wakipelekwa
hospitali kwa matibabu kutokana na kuvuja damu nyingi iliyosababishwa
na majeraha ya risasi waliyoyapata. Miili ya marehemu imehifadhiwa
katika chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.”
Kamishna
Sabas amesema katika tukio hilo wamefanikiwa kupokonya silaha mbili
aina ya SMG na Shotgun moja pamoja na risasi tisa.
Kamishina
Sabas amewataka wananchi kutoa taarifa zitakazowezesha kupatikana kwa
wahalifu wengine waliosalia na kwamba zawadi nono bado ipo pale pale
na itatolewa kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa sahihi kuhusiana na
wahalifu wanaojihusisha na mauaji katika kanda maalumu ya Rufiji.
0 Maoni:
Post a Comment