Manchester United wamewapiku Chelsea
na kumsajili mshambuliaji wa Everton Romelu Lukaku, 24, kwa kutoa
kitita kitakachovunja rekodi ya dunia cha pauni milioni 75 (Daily Mail).
Manchester United wangependa kumsajili kiungo wa Borussia Dortmund Julian Weigl baada ya kushindwa kuwapata Eric Dier kutoka Tottenham na Nemanja Matic kutoka Chelsea (Daily Mail).
Paris St-Germain wapo tayari kutoa pauni milioni 70 kutaka kumsajili kiungo wa Liverpool Philippe Coutinho, 25 (Le10 Sport).
Atletico Madrid wanajiandaa kutoa dau rasmi la pauni milioni 22 kutaka kumsajili Diego Costa, 28, kutoka Chelsea (Guardian).
Chelsea wamefikia makubaliano na Roma ya kumsajili beki Antonio Rudiger, 24 kwa pauni milioni 34, ingawa mchezaji huyo bado hajafikia makubaliano rasmi kuhusu maslahi binafsi (Sky Sports).
Meneja wa zamani wa Liverpool Gerard Houllier anasema Arsenal huenda wamempata 'Ian Wright mpya' baada ya kumsajili Alexandre Lacazette (TalkSport).
Mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez, 28, anataka mshahara wa pauni 400,000 kwa wiki, ambao ni ongezeko la pauni 125,000 kwa wiki katika mshahara wake wa sasa (Daily Mirror).
Arsenal wametoa dau jipya kwa Monaco kutaka kumsajili winga Thomas Lemar (Evening Standard).
West Ham wanaonekana kuongoza katika mbio za kutaka kumsajili mshambuliaji wa Burnley Andre Gray, 26, kwa pauni milioni 15 (Evening Standard).
Huddersfiled waliopanda daraja EPL wanakaribia kumsajili beki Mathias Jorgensen, 27, kutoka FC Copenhagen kwa pauni milioni 3.5 (Sun).
Kiungo wa Chelsea Nathaniel Chalobah, 22, anazungumza na Watford kutaka kuhamia katika timu hiyo aliyoichezea kwa mkopo msimu wa 2012-13 (Daily Mirror).
Dau la pauni milioni 3 la Burnley la kumtaka mshambuliaji wa Stoke City Jonathan Walters limekubaliwa (Sky Sports).
Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii (Kwa Kiingereza): Uhamisho wa wachezaji Ulaya
Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Uwe na siku njema.
0 Maoni:
Post a Comment