Chama
tawala nchini Uganda cha National Resistence Movement (NRM) kimeapa
kuhakikisha kwamba katiba ya nchi hiyo ina badilishwa ili kumruhusu Rais
Yoweri Museveni kuitawala Uganda hadi mwisho wa umri wake.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyochapishwa leo katika mtandao wa Idhaa ya
Kiswahili VOA inaeleza kuwa, NRM, imetangaza kutumia mbinu zote
kuhakikisha kwamba katiba ya nchi inabadilishwa ili kumruhusu Rais
Museveni kutawala hadi kifo chake. Hata hivyo Wanasiasa wa upinzani nao
wameapa kuzima kila jaribio la kuifanyia katiba marekebisho.
Taarifa
hiyo imeongeza kuwa, japokuwa Museveni amekaa kimya, viongozi wa NRM,
wanasema wanasiasa wa upinzani wanamaliza muda wao kupinga nia ya chama
tawala kuondoa ibara ya 102 B inayomzuia mtu yoyote aliyetimiza umri wa
miaka 75 kuwania madaraka ya urais.
Viongozi
hao wanaongozwa na mshauri wa Rais, David Mafabi ambaye amesema kuwa:
“Hakuna wasiwasi kuhusu hilo. Tunataka katiba ibadilishwe na tunaieleza
dunia ijue. wanaopinga wachunguze.
Kulingana
na viongozi wa chama cha NRM, umri hauwezi kuwa kizuizi kwa kiongozi
aliye na uwezo wa kuingoza nchi, na kwamba hakuna mtu yeyote nchini humo
anayeweza kuwa rais isipokuwa Yoweri Kaguta Museveni.
Wanasiasa
wa upinzani wakiongozwa na Dkt Kiiza Besigye wa FDC na Nobert Mao, kwa
upande wao, wameendeleza kampeni ya kutaka raia kususia jaribio la
serikali kuifanyia marekebisho katiba wakitishia kutumia mbinu zote
kuzima hatua hiyo.
Katiba
ya Uganda ilifanyiwa mabadiliko mnamo mwaka 2005 na kuondoa kizuizi cha
mihula miwili, iliyomwezesha Museveni kuwania urais kwa mara nyingine.
Museveni ameitawala Uganda tangu mwaka 1986.
0 Maoni:
Post a Comment