Waziri
Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amewasili leo, Julai 20 saa mbili
asubuhi makao makuu ya Jeshi la Polisi kwenye ofisi za Mkurugenzi wa
Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Boaz.
Lowassa ameambatana na mkewe, Regina na mwanasheria wake, Peter Kibatala.
Hii
ni mara ya nne kwa Lowassa kuripoti hapo akituhumiwa kutoa kauli za
kichochezi wakati wa futari iliyoandaliwa Juni 23, na Mbunge wa Ukonga,
Mwita Waitara.
Katika
futari hiyo, Lowassa anadaiwa kutoa maneno ya uchochezi kuhusu masheikh
wa Taasisi ya Uamsho wanaoshikiliwa gerezani akidai utaratibu wa
kisheria ufanyike ili waachiwe huru.
Polisi wameimarisha ulinzi eneo hilo, huku Lowassa akiwa ndani tayari kwa kuhojiwa.
0 Maoni:
Post a Comment