Rais
John Magufuli amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela
kuyafanyia kazi malalamiko ya mwanamke mmoja mkazi wa Sengerema aliyedai
kunyanyaswa na kuvunjiwa nyumba yake.
Rais
ametoa agizo hilo leo (Jumanne Julai 4) wakati akizindua mradi wa maji,
wilayani Sengerema na kumtaka Mongela kuchukua namba ya simu ya
mwanamke huyo aliyejitambulisha kwa jina la Rosemary Simon, ili
atatuliwe tatizo lake.
Kabla
ya Rais Magufuli kuchukua hatua hiyo, mwanamke huyo alikwenda mbele ya
jukwaa alimoketi Rais, huku akilia kuwa ananyanyaswa na viongozi wa
Chadema na kuwa wanataka kumbomolea nyumba yake, bila kufafanua ni kwa
vipi.
“Mpe
simu yako Mkuu wa Mkoa, halafu atakutafuta na wala usijali, nitamtuma
Mkuu wa Mkoa na haki yako itatendeka, nitalifanyia kazi suala lako,” amesema Rais.
0 Maoni:
Post a Comment