Liverpool yashinda Kombe la Asia dhidi ya Leicester

Liverpool yaishinda Leicester 2-1Liverpool yaishinda Leicester 2-1 

Liverpool iliibuka mshindi wa kombe la Asia awamu ya 2017 mbele ya mashabiki wengi wa timu hiyo mjini Hong Kong.

Mohamed Salah na Phil Coutinho walifunga mabao mawili mazuri na kuishinda Leicester waliokuwa wamefunga bao la mapema.

Huku kukiwa na uvumi kwamba Coutinho huenda akajiunga na Barcelona haikutarajiwa kwamba nyota huyo wa Liverpool angefunga bao la ushindi.

Mechi ilikuwa na kipindi cha kwanza cha kutumbuiza huku washambuliaji wote wa timu hizo wakishiriki.

Coutinho na Salah walikuwa wakionana kwa kipindi kirefu cha mechi.

Leicester ndio ilioanza kufunga baada mchezaji Fuchs kutumia wingi ya kulia kabla ya kupiga krosi nzuri kwa Isaac Slimani ambaye alifungakwa kichwa katika dakika ya 12 kipindi cha kwanza


Share on Google Plus
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment