Mkuu
wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro amesema siku zinahesabika kwa
wahalifu wote waliojificha mkoani Pwani ambao wamekuwa wakifanya matukio
ya uhalifu ikiwa pamoja na kufanya mauaji kwa baadhi ya viongozi na
askari polisi nchini.
IGP
Sirro amesema hayo jana alipokuwa katika ukumbi wa Police Officer's
Mess, Oysterbay Dar es Salaam wakati akikabidhiwa magari manne na
kampuni ya kichina ya Great Wall Motors and Haval na kudai kuwa magari
hayo yatasaidia kupambana na uhalifu nchini.
"Si kawaida yangu kusema sema ila muda si mrefu nitatoa majibu ya mauaji ya Pwani" alisema Simon Sirro
Pia
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya kichina ya Great Wall Motors and
Haval alisema msaada huo wa magari ambao wameutoa kwa jeshi la polisi
nchini ni sehemu ya kuunga mkono juhudi kubwa za jeshi hilo katika
kupambana na uhalifu nchini.
Mpaka
sasa ni zaidi ya watu 30 wamepoteza maisha mkoani Pwani kwa kuuliwa na
watu wasiojulikana huku wengine kadhaa wakiwa wamejuruhiwa kwa risasi na
watu hao.
0 Maoni:
Post a Comment