Victoria Azarenka
Mcheza tenesi Victoria Azarenka
amerejea uwanjani na kuanza vibaya baada kushindwa kutamba mbele ya
Mjapani, Risa Ozaki, na ukiwa ndio mchezo wa kwanza kwa Azarenka, baada
ya kuwa nje ya mchezo kwa muda wa mwaka mmoja.
Azarenka ambae
hajacheza toka mwaka 2016, mara ya mwisho alishiriki michuano ya wazi ya
Ufaransa, alianza vizuri mchezo dhidi ya Ozaki, ambapo aliongoza kwa
6-3 kabla ya kupoteza kwa 6-4, 5-4 katika mchezo wa raundi ya kwanza.
Mcheza tenesi huyu alipumzika kwa muda kucheza mchezo huo baada ya kujifungua mtoto mnamo mwezi Desemba mwaka jana.
Azarenka baada ya michuano ya Mallorca atashiriki michuano ya wazi ya Wimbledon itayofanyika mwezi ujao.
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
0 Maoni:
Post a Comment