James Clapper, mkuu wa zamani wa Shirika la Kijasusi la Marekani, CIA
Katika kile kinachoonekana wazi ni kuzidi
kuongezeka mzozo baina ya Marekani na Russia, mkuu wa zamani wa Shirika
la Kijasusi la Marekani CIA amesema kuwa, Russia ina mikakati ya muda
mrefu ya kujipenyeza katika safu za viongozi wa Marekani kwa ajili ya
kuwadhibiti.
James Clapper amesema hayo katika
mahojiano aliyofanyiwa na televisheni ya NBC News kuhusiana na tuhuma
zinazomkabili Jared Kushner, mkwe wa rais wa Marekani, Donald Trump
anayedaiwa kuwa na uhusiano na Russia na kusema kwamba, hata yeye
alikuwa na taarifa hizo tangu zamani na alionya kuwa Warussia
wanaingilia uchaguzi wa Marekani.
Rais wa Marekani Donald Trump akipeana mkono na mkwewe, Jared Kushner
Mkuu wa zamani wa Shirika la Kijasusi la
Marekani CIA ameongeza kuwa, kwa kawaida Russia huwa wanajiweka chini
ya baadhi ya watu, kujipenyeza kwenye fikra na mambo yao na kushirikiana
nao ili wawaunge mkono.
Amesema, mbinu waliyotumia Warussia
katika uchaguzi uliopita nchini Marekani ilikuwa ni kueneza habari za
uongo hasa kwenye mitandao ya kijamii na kuingilia moja kwa moja
uchaguzi huo.
Mkuu huyo wa zamani wa CIA ameituhumu
Russia kuwa inaingilia masuala ya kisiasa ya Marekani na kuitaka
Washington iiwekee vikwazo Moscow.
0 Maoni:
Post a Comment