Mwili
wa Mzee Francis Maige Kanyasu alimaarufu kwa jina la Mzee Ngosha ambaye
anayetajwa kuwa ni moja wa wachoraji wa nembo ya Taifa aliyefariki
tarehe 30 mwezi wa 5 unatarajiwa kusafirishwa leo kuelekea Misungwi
Mwanza.
Kwa
mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu Wizara ya Afya (Maendeleo ya Jamii)
imesema kuwa ndugu wa Mzee Kanyasu wamepatikana na sasa serikali
itagharamia kusafirisha mwili wa mzee huyo mpaka Mwanza ambapo atakwenda
kuzikwa huko.
Mwili
wa Mzee Francis Maige unatarajiwa kuagwa leo Jumamosi saa 2 asubuhi
Hospitali Taifa ya Muhimbili kabla ya kuanza safari ya kuelekea Mwanza.
0 Maoni:
Post a Comment