Real Madrid na Manchester United waoneshana ubabe kifedha.

Hiki ni kiburi kikubwa ambacho United wameamua kuwaonesha Real Madrid, ni sawa na kusema United hawataki chochote kile toka kwa Real Madrid bali wanataka waachane na wachezaji wao.

Dau la £60m ambalo Real Madrid wamelituma kwa Manchester United kumtaka David De Gea ni kubwa sana haswa kwa nafasi anayocheza David De Gea na ni wazi hii ilikuja kama bahati.

Lakini huwezi kuamini kwani Manchester United wamesema hapana na hawako tayari kupokea kiasi hicho cha fedha kwani David De Gea hauzwi kwa kiasi chochote kile na mpango wao ni abaki klabuni hapo.

Haitakuwa rahisi kwa Real Madrid kukubali kushindwa kwani ni timu ambayo mara zote imekuwa kama inahitaji mchezaji yoyote yule huwa wanamchukua hata kwa gharama kiasi gani.

Na David De Gea amekuwa mchezaji ambaye wanamtaka sana na kwa hakika watarudi tena na ofa mpya ambayo wanahisi inaweza kuishawishi United kumuuza De Gea.
Share on Google Plus
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment