Hizi anazofanya Pep Gurdiola sokoni sasa ni fujo

Baada ya msimu wa ligi kuisha kulitembea ufagio katika klabu ya Manchester City na wachezaji kadhaa kuoneshwa mlango wa kutokea, hii ilimaanisha City wanaenda kujijenga upya kwa kuleta wachezaji mpya.

Baada ya dirisha la usajili tu kuanza Gurdiola akawapiga bao Real Madrid na Manchester United kwa kumnunua kiungo wa Monaco Bernardo Silva kwa dau la £43m.

Baada ya kumnunua Bernardo Silva siku kadhaa baadae ndani ya wiki moja Gurdiola kahamia kwa golikipa wa Benfica Ederson ambapo anatarajia kuwa golikipa ghali katika ulimwengu huu wa soka.

Gurdiola amepewa jina jipya la “Mr Cheque Book” jina ambalo amelipewa siku za hivi karibuni kutokana na pesa anazomwaga tu kwa kila mchezaji ambaye anamtaka.

Wakati suala la golikipa Ederson likikamilika tayari habari mpya kutoka familia za mwanasoka anayekipiga katika klabu ya Monaco Benjamin Mendy amekubali kujiunga na klabu ya Manchester City.

Picha za Mendy akiwa katika ndege binafsi siku ya Junapili inahisiwa alikuwa akienda Uingereza ili kukamilisha taratibu za mwisho za usajili wake kwenda Manchester City.
Share on Google Plus
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment