Mbunge wa Kibamba kupitia CHADEMA, Mhe. John Mnyika, ametolewa nje ya bunge kwa nguvu na askari mara baada ya kukiuka kanuni na taratibu za Bunge.
Hata hivyo, kitendo hicho kimeonekana kuwachukiza Wabunge wa kambi ya upinzani bungeni na kuamua kususia kikao na kutoka nje ya Bunge.
Lakini katika hali isiyo kuwa ya kawaida wakati wabunge hao wakitoka, ni Mbunge mmoja tu wa Kambi ya Upinzani Mhe Maftaha Nachuma wa Mtwara Mjini kupitia chama cha CUF aliyebaki mwenyewe kuendelea na kikao.
Spika wa Bunge, Job Ndugai amewaamrisha askari wamtoe kwa nguvu Mbunge huyo mara baada ya majibizano makali na Mhe Livingstone Lusinde Mbunge wa Mtera. Spika Ndugai amemuonya Mnyika afuate utaratibu lakini akaaendelea kujibizana ndipo alipoamrisha askari wamtoe nje kwa nguvu na wametekeleza amri hiyo.
0 Maoni:
Post a Comment