Ligi ya vilabu bingwa barani Ulaya inatarajiwa kufikia tamati hii leo mara baada ya kuwakutanisha miamba wawili wa soka barani humo klabu ya Real Madrid kutoka Hispania na Juventus ya Italy.

Aidha, katika mechi hiyo iliyoteka hisia za wengi makocha wa pande zote mbili wametambiana kuibuka na ushindi katika mchezo huo wa fainali ya mabingwa barani humo.

“Timu yangu iko vizuri na wachezaji wako imara na wana ari ya kutosha hivyo, naimani tutaibuka na ushindi kwenye mchezo huu ukizingatia historia inajieleza kwakuwa na muendelezo mzuri,”amesema kocha wa Real Madrid, Zidane.

Kwa upande wake kocha wa Juventus, Max Allegri amesema kuwa wachezaji wake wako vizuri na anamatumaini makubwa ya kuibuka na ushindi katika fainali hiyo ambayo itakuwa ni ya aina yake.