Baada ya Leseni ya Magari Kufutwa..Polisi Waagizwa Kuyaachilia Magari Yote Yaliyokamatwa kwa Kutokuwa na Leseni..!!!

 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba ametoa agizo kwa Jeshi la Polisi nchini kuyaachia magari yote ambayo yanashikiliwa na Jeshi hilo kwa kosa la kutolipia ada ya mwaka ya leseni ya magari.

Waziri Mwigulu ametoa agizo hilo baada ya Serikali kufuta ada hiyo ambayo italipwa mara moja tu gari litakaposajiliwa.

Serikali imetangaza kufuta ada hiyo pamoja na kutoa msamaha wa kodi, riba na adhabu zinazoambatana na madeni yote (Tax Amnesty) ya ada hiyo yaliyolimbikizwa kwa miaka ya nyuma.
Share on Google Plus
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment