Jaji CS Karnan
Aliyekuwa hakimu wa zamani wa
mahakama kuu nchini India amepelekwa lupango Mashariki mwa mji wa
Kolkata, siku moja baada ya kukamatwa kwake Kusini mwa mji wa Tamil
Nadu.
Jaji Karnan kwa sasa amevuliwa mamlaka yake ya mahakama. Na inaelezwa kuwa ndiye jaji wa kwanza nchini humo kutoka mahakama kuu kuhukumiwa na kufungwa jela.
Jaji huyo alihojiwa baada ya kumwandikia waraka waziri mkuu,baada ya matamshi yake dhidi ya majaji wenziwe wa mahakama kuu kuwa ni wala rushwa waliopitukia.
0 Maoni:
Post a Comment