Halmashauri ya Geita yakabiliwa na upungufu wa damu salama

Halmashauri ya mji wa Geita yenye Vituo Viwili vya Afya pamoja na Zahanati nne inakabiliwa na uhaba wa damu salama chupa 95 kwa mwezi hali inayotishia maisha ya wagonjwa wakiwemo watoto chini ya miaka mitano na wajawazito wakati wa kujifungua kutokana Jamii kutohamasika kuchangia damu salama.

Kufuatia hali hiyo, Waumini wa Makanisa 14 ya Wadventista Wasabato yanayounda Mtaa wa Mbugani wameadhimisha siku Muhimu ya Matendo ya Huruma kwa kuchangia Damu kuokoa maisha ya wagonjwa kwenye vituo hivyo vya Afya pamoja na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita.

Mchungaji wa Mtaa wa Mbugani Elias Emanuel Kahibi anasema lengo la zoezi hilo ni kusaidia kuokoa Maisha ya Wagonjwa walioko Hospitalini wanaohitaji damu,huku akiwatoa wito kwa jumuiya hiyo na jamii nzima kujitokeza kuchangia damu.

Zoezi hilo limefanyika ikiwa ni siku ya Sabato ya 23, siku ambayo waumini wa kanisa hilo huadhimisha nguzo muhimu ya matendo ya huruma.

Baadhi ya waumini walioshiriki zoezi hilo wakazungumzia umuhimu wa kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa.

Aidha,mhamasishaji wa Timu ya Ukusanyaji damu damu salama Halmashauri ya Mji wa Geita Prisca Rupia amesema mahitaji ya damu salama kwa mwezi ni chupa 125 lakini kutokana na changamoto mbalimbali chupa zinazopatikana kwa mwezi ni 30 tu hali inayotishioa maisha ya wagonjwa
Share on Google Plus
Ahsante kwa kutembelea site yangu, unaweza kunicheki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubonyeza icons juu kulia na kunipata moja kwa moja kwenye Facebook, Twitter na Instagram...Endelea kuwa karibu yangu ili uweze kufikiwa na chochote kinachonifika.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment