Msanii wa Bongo Fleva, AY amesema kuna faida na harasa kwa msanii kufanya remix ya wimbo wake ambao umesha-hit.
Rapper ameeleza kwanza msanii kufanya remix ya wimbo ambao umesha-hit ni jambo la kujilipua sana ndio maana wasanii wengi wanaogopa kufanya hivyo kwa sababu wanaweza wakaua wimbo huo.
“Ukitoa wimbo uka-hit halafu ukatoa remix isi-hit unaua ule wimbo wa kwanza, na kufanya remix ni wewe mwenywe kujikosoa kwa kusema sikufikia kiwango ambacho kinatakiwa ngoja niuboreshe zaidi huu wimbo wangu,” AY amekiambia kipindi cha Dj Show cha Radio One.
“Na kingine unataka kuonyesha watu huu wimbo mlioupenda na mliufanya moja ya wimbo mkubwa lakini naweza kuonyesha uwezo mwingine kwa kuubadilisha ili kuelekea katika picha nyingine ambayo mtaupenda zaidi,” ameongeza.
AY ameeleza faida nyingine kwa msanii kufanya remix na kuwakutanisha wasanii wengine ni kuonyesha mashabiki kuwa tunaweza kufanya kolabo, na hili linaweza kuchochewa na wasanii ambao wanakuwa karibu na msanii husika.
0 Maoni:
Post a Comment