Asasi zisizo za kiserikali zimeonya kuhusiana na kuendelea kuwa mbaya hali ya wakimbizi na mgogoro wa kibinadamu nchini Chad.
Taarifa ya asasi hizo imeeleza
kuwa, wakimbizi huko Chad wanakabiliwa na hali mbaya ya kibinadamu na
kwamba, kuna haja ya kuchukuliwa hatua za haraka za kuwasaidia ili
kuepusha kutokea maafa ya kibinadamu.
Pierre Valiquette, mkuu wa moja ya asasi
za kiraia nchini Chad sambamba na kutahadharisha kuhusiana na kuendelea
mgogoro wa wakimbizi huko Chad amesema kuwa, takribani wakimbizi wote
walioko nchini humo wanahitajia misaada ya kibinadamu hususan chakula.
Hivi karibuni Umoja wa Mataifa
ulitangaza kuwa, kumetengwa bajeti maalumu ya kuwasaidia wakazi wa eneo
la Ziwa Chad ambao kwa sasa wanakabiliwa na hali mbaya kimaisha.
Stephen O'Brien, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya kibinadamu
O'Brien, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya kibinadamu na mratibu wa misaada ya kibinadamu amesema kuwa, umoja huo umetenga bajeti ya dola 3.5 kwa ajili ya kuwasaidia wakazi wa Ukanda wa Ziwa Chad wanaotatizika kudhamini mahitaji yao ya lazima ya kila siku.
Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa
Mataifa watu milioni 11 katika eneo la Ziwa Chad linalojumuisha
Cameroon, magharibi mwa Chad, kusini mashariki mwa Niger na kaskazini
mashariki mwa Nigeria wanahitajia misaada ya haraka ya chakula.
0 Maoni:
Post a Comment